• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Tabora Vijijini
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

BILIONI 5.4 KUJENGA BARABARA ZA TARURA MKOANI TABORA

Posted on: November 25th, 2020

JUMLA ya shilingi bilinoni 5.4 zinatarajiwa kutumika katika ukarabati na utengenezaji wa barabara za Mkoa wa Tabora ambazo ziko chini ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA)

Kauli hiyo imetolewa  na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt.Philemon Sengati wakati wa sherehe fupi ya kusaini mikataba ya ujenzi na ukarabati wa barabara kwa Wakandarasi na TARURA.

Alisema kiasi hicho ni awamu ya kwanza ya kiasi cha shilingi bilioni 7.1 iliyoidhinishiwa TARURA kwa mwaka wa fedha wa 2020/21 kwa ajili ya matengenezo ya barabara.

Dkt. Sengati alisema kazi zitakazofanyika ni pamoja na ujenzi wa kilimote 2.76 kwa kiwango cha lami , ujenzi wa makaravati zaidi ya mistari 59 na uchongaji wa barabara zaidi ya kilometa 541.

Aliwasihi Wakandarasi 34 walioshinda zabuni ya kutengeneza na kukarabati barabara hizo kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria , kanuni na miongozo , ubunifu na weledi ili Serikali iendelee kuwa na imani nao na kuwapa kazi zaidi.

“Wakandarasi walioomba kazi ni wengi lakini nyie 34 tu ndio mmefanikiwa kupata nafasi …kwa hiyo msituangashe …tangulizeni mbele uzalendo kwa maslahi mapana ya Mkoa wa Tabora na Taifa kwa ujumla” alisisitiza.

Aliwataka Wakandarasi walioshinda kazi hiyo kuhakikisha kazi inakamilika ndani ya muda uliopangwa na kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha iliyotolewa na Serikali.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alimwagiza Mratibu wa TARURA na Wataalamu wake kuhakikisha wanasimamia kwa karibu miradi yote iliyopangwa ili ikamilike kwa viwango vilivypangwa.

Alisema Serikali inatoa fedha nyingi kwa miradi ya barabara , hivyo hatasita kumchukulia hatua Mtumishi ambaye atasababisha miradi kutekelezwa chini ya kiwango kwa kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo.

Dkt. Sengati alisema ujenzi wa miundombinu hiyo na mingine itachochea maendeleo katika sekta za utalii,  kilimo.mifugo, uvuvi , viwanda na biashara.

Alisema hatua hiyo itasaidia kuimarisha kipato cha wakazi na Mkoa  kwa ujumla na kufikia maono ya miaka mitano ijayo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ya kukuza uchumi kwa wasatani wa asilimia 8 .

Matangazo

  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha Kwanza 2021 Shule za Sekondari za Serikali December 18, 2020
  • Fomu ya Kujiunga Kidato cha kwanza, 2021 kwa shule za Mkoa wa Tabora December 16, 2020
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2020 November 23, 2020
  • NAMBA ZA MAWASILIANO OFISI YA MKOA TABORA November 23, 2020
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MIFUKO 462 YA MBOLEA YA TUMBAKU YA CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA MILAMBO ILIYOKUWA IMEPOTEA IMEPATIKANA

    December 30, 2020
  • RC AWATAKA WALIMU WAKUU KUJENGA UMOJA KWA WALIMU WALIOCHINI YAO

    December 30, 2020
  • POLISI WANASA WATUHUMIWA 683 MKOANI TABORA WA MAKOSA MBALIMBALI NDANI YA WIKI TATU

    December 30, 2020
  • RC ATOA SIKU 38 VETA KUKAMILISHA UJENZI WA CHUO CHA UYUI NA IGUNGA

    December 24, 2020
  • Angalia zote

Video

JPM BANDARINI
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • Government Portal
  • SALARYSLIP

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa