BODA BODA TABORA WAFURAHIA KUINGIZWA KWENYE BIMA YA AFYA
UMOJA wa Madreva wa Bajaji na pikipiki(boda boda) Mkoani Tabora wameipongeza Serikali kwa kuwasaidia kuingia katika Mfumo wa kupata huduma za matibabu kupitia Bima ya Afya.
Hatua hiyo itasaidia kuokoa maisha yao wanapopata matatizo mbalimbali ikiwemo wanapopata ajali na wakati mwingine kuugua.
Kauli hiyo imetolewa jana na Makamu Mwenyekiti wa Madreva Bajaji Waziri Kipusi wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ya kuwahamasisha Madereva Bajaji na Bodaboda kujiunga na Bima ya Afya.
Alisema kabla ya kuanza kwa utaratibu huo haujaanza walikuwa wakilazimika kusema uongo ili wenzao waliopata ajali wapate matibabu.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa Aggrey Mwanri aliwataka Vijana wote wanaojihusisha na usafirishaji wa abiria kwa kutumia Bajaji na Pikipiki maarufu kama bodaboda kuchangamkia fursa hiyo iliyotolewa kwao na Serikali ya awamu ya tano.
Alisema kupitia utaratibu huo watanufaika kwa kupata huduma za Bima ya afya kwa kuchangia shilingi 100,000/- kwa mwaka badala ya ule wa mtu mmoja kulipa shilingi 1.5 kwa mwaka ili kupata huduma hizo.
Mwanri alisema Serikali imeamua kuwapunguzia mzigo kwa wale Bodaboda na Bajaji ambao watakuwa wako katika umoja ili waweze kupata huduma za afya kwa gharama nafuu.
Naye Meneja wa Bima ya Afya Mkoa wa Tabora Adam Salum alisema siku za nyuma Mfuko wa Bima ya Afya ulikuwa ukihudumia watumishi wa umma pekee lakini hivi sasa umeiongia makundi mbalimbali kama vile Wajasiriamali , Umoja wa Boda boda na Bajaji.
MWISHO
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa