KAMATI ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora imewaagiza Wataalamu wa sekta ya kilimo kuwahamasisha wakulima zao la Karanga ili kupunguza upatikanaji wa mafuta ya kula hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo Wilayani Kaliua na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi wakati wa ziara ya Kamati kukagua miradi ya maendeleo,
Alisema wakati Serikali ikihimiza na kuwahamasisha kilimo a;izeti na michikichi ili kukabiliana na upungufu wa mafuta ya kula ni vema wakaongeza na Karanga ambalo nalo linazalisha mafuta.
Wakasuvi alisema kuwa uzalishaji mkubwa wa zao hilo utasaidia kupunguza tatizo la mafuta kwa watu ambao watakuwa wakitumia Karanga watapunguza matumizi ya mafuta ya aina nyingine na hivyo kupelekwa katika maeneo yenye upungufu.
Alisema mbali na matumizi katika mboga zao hilo lina bei kubwa ukilinganisha na mahindi na mpunga na hivyo linaweza kipato mkulima.
Wakasuvi alisema kuwa debe moja karanga za maganda linauzwa shilingi 10,000/=, mpunga na mahindi shilingi 5,000/= kila moja.
Aliongeza bado zao hilo mkoani Tabora gharama zake za uzalishaji sio kubwa kwa kuwa haitaji pembejeo na linakubali katika maeneo mengi.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa CCM ameiomba Serikali kusaidia tatizo la mbolea kupanda bei kwa kuwa linaweza kusababisha kupungua kwa uzalishaji msimu ujao.
Alisema hivi sasa mbolea zimepanda na muda wa kilimo umekaribia na upo uwezekano wa wakulima wakashindwa kuzinunua.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa