WAZAZI na Walezi katika Manispaa ya Tabora wameombwa kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao ili waweze kupata mlo wakati wakiwa shuleni.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Alisema hatua hiyo itasaidia kuongeza ufaulu kwa watoto kutokana na kuhudhuria masomo wakati wote.
Dkt.Nawanda alisema katika Manispaa ya Tabora upatikanaji wa mahindim mpunga ni mzuri nakuwaomba kutumia sehemu ya chakula wanachovuna kutenga kwa ajili ya watoto wawapo shuleni.
Mkurugenzi |Mtendaji wa Manispaa ya Tabora Dkt. Peter Nyanja alisema wazazi wanaweza kuweka utaratibu mzuri wa kuchangia debe moja na mahindi, moja la mpunga na maharage kilo 10 na shilingi 1,000 za gharama za mpishi kwa kila mzazi
Aliongeza kuwa wakifanikisha hilo Manispaa itawasaidia katika ununuzi wa sukari na vitu vingine.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda amewashauri wananchi kujenga tabia ya kufuga kuku kama sehemu ya mradi wa kuwaingizia kipato cha haraka.
Alisema kila kaya ikianza na kuku 10 baada ya miezi sita zitakuwa zimeongezeka na kufikia zaidi ya 100.
Dkt.Nawanda baada ya kipindi hicho kila kaya inakuwa na uhakika wa kupata shilingi 750,000 kupitia uuzaji wa mayai na kuku ambazo ni sawa na mshahara wa ajira ya kwanza kwa Mhitimu wa Chuo Kikuu.
Alisema uongozi wa wilaya utandaa utaratibu wa kuwatafutia chanjo ili kuhakikisha kuku wao hafi kwa uongojwa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa