• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

ISAWIMA YAKABIDHIWA KWA TAWA ILI KUDHIBITI UHARIBIFU

Posted on: January 25th, 2021

ISAWIMA YAKABIDHIWA KWA TAWA ILI KUDHIBITI UHARIBIFU

HATIMAYE Serikali imekabidhi usimamizi wa eneo la Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima lilipo wilayani Kaliua kwa  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ili kukomesha uharibifu maliasili ikiwemo ukataji magogo na uwindaji haramu wa wanyamapori unaofanyika katika eneo hilo.

Hatua hiyo inafuatia Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima kushindwa kudhibiti vitendo vya uharibifu na mauaji ambayo yanaendelea ndani ya Hifadhi hiyo.

Makabidhiano ya awali yamefanywa  na Mkuu na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuwapa TAWA ili waweze kuanza kazi ya kulinda Hifadhi hiyo.

Alisema Serikali imechukua hatua hiyo baada ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima kutokamilisha taratibu za usajili na kutokuwa na uwezo na  nguvu za Kisheria za kuisimamia hifadhi hiyo hali iliyopelekea kuendelea kwa ujangili, mauaji na kusababisha tishio kubwa la kutowekwa kwa Hifadhi hiyo.

Dkt. Sengati alisema Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Isawima haina rasilimali za kutosha kukabiliana na uharibifu katika eneo hilo na hivyo kufanya kuwepo kwa makundi ya wavamizi ndani ya mistu.

Alisema kufuataia kukosekana kwa rasilimali vitu na watu wamekuwa wakingonja uharibifu utokee ndio waende kwa ajili ya kujipatia fedha toka kwa waharifu zinazotokana na uuzaji wa magogo na faini ,badala ya kufanya kazi ya kuzuia uharibifu kwa ajili ya uendelevu wa maliasili hiyo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Dkt. Sengati alisema mtindo huo wa usimamizi umesababisha kuzuka kwa migogoro ya mara kwa mara ambayo kwa upande mwingine imesababisha hata watu kupoteza maisha.

Aliwataka TAWA baada ya kupewa jukumu hilo ,kufanyakazi kwa uzalendo katika kulinda rasilimali hiyo muhimu kwa wakazi wa mikoa ya Tabora na Kigoma ili Serikali isije ikaona kuwa imekosea kuwapa jukumu la usimamizi.

Dkt. Sengati aliongeza kuwa katika usimamizi ni vema wakaendelea kushirikiana na vijiji vilivyotoa ardhi yao kwa ajili ya uanzishaji wa Hifadhi hiyo ili nao waone manufaa ya kuwepo kwake.

Alisema wanaweza kuwashirikisha kwa kuwaruhusu kufanya shughuli ambazo haziathiri uhifadhi kama vile ufugaji wa nyuki katika eneo la Hifadhi  na kutoa michango kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo kama vile kuwajengea shule na Zahanati sehemu ambazo hawana.

Dkt. Sengati aliwataka kufanyakazi katika kuhakikisha wavamizi wote na vikundi vyote vya uhalifu vilivyomo ndani ya msitu huo vinaondoka ili uharibifu usiendelee.

Alisema lengo la Serikali ni kutaka msitu huo hatimaye uje upande kwa ajili ya kuongeza mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua na Taifa kwa ujumla.

MWISHO

 

 

 

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MHE. CHACHA AIPONGEZA TIMU YA UMISSETA MKOA KWA KUSHIKA NAFASI YA TATU KITAIFA

    July 01, 2025
  • RC. CHA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WAPYA, WAAHIDI KUFANYA KAZI KWA BIDII NA UADILIFU.

    July 01, 2025
  • TABORA: MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATAKIWA KUZINGATIA SHERIA NA MAADILI YA NCHI

    June 26, 2025
  • MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA YAENDESHA MAFUNZO MAALUM YA MATUMIZI YA MFUMO WA PEPMIS KWA WATUMISHI WA UMMA MKOA WA TABORA

    June 23, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa