• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

MAJENGO YA HOSPITALI YA MANISPAA YAKAMILIKE KATIKA KIPINDI HUSIKA-RC TABORA

Posted on: July 9th, 2020

UONGOZI wa Manispaa ya Tabora umetakiwa kuhakikisha Wakandarasi wanaojenga majengo ya  Hospitali ya Wilaya na yale ya Kituo cha Afya Tumbi wanakamilisha kwa ubora unatakiwa na ya  muda waliopewa katika mkataba ili wananchi waweze kupata huduma kwa karibu.

Kauli hiyo imetolewa  na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kukagua miradi ya maendeleo.

Alisema kiasi cha shilingi milioni 700 zilizotolewa na Serikali ni lazima zionekane katika miundo mbinu itakayojengwa na iwe msaada kwa wananchi kupata huduma bora kwa gharama nafuu.

Dkt. Sengati alisema hatasita kuwachukulia hatua watendaji wote watakaobainika kutumia fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo wananchi wayonge kwa maslahi binafsi.

Aliwataka watendaji wanaopewa majukumu ya kusimamia miradi kuwa wazalendo na waaminifu ili siku moja nao wawe sehemu ya mafanikio hayo.

Naye Katibu wa Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Tabora Joseph Kashushula alisema Mwezi Mei mwaka huu walipokea shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa majengo matatu ambapo yote yameanza.

Alisema majengo hayo ni Jengo la Wagonjwa wa Nje(OPD), Maabara na kichoma taka  na yote yanatarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu kama ilivyo kwenye mkataba.

Kashushula alisema kiasi hicho ni sehemu ya fedha za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambapo ndani ya mwaka wa fedha huu wanatarajia kupata kiasi cha shilingi bilioni 1 ili kukamilisha majengo ambayo yatakuwa yamebaki.

Kwa upande wa Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Tumbi Charles Ngussa alisema walipokea kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo wa Nje (OPD) na vyoo.

Alisema hadi hivi sasa wameshatumia shilingi milioni 113.1 na zimebaki shilingi milioni 86.8.

Ngussa alisema kati ya fedha zilizotumika wameweza kununua vifaa vyote vinatakiwa ikiwemo bati na rangi.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora mara baada ya kuwasili ofisini kwake jana alianza kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa dhana ya hapa kazi.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MHE. CHACHA AIPONGEZA TIMU YA UMISSETA MKOA KWA KUSHIKA NAFASI YA TATU KITAIFA

    July 01, 2025
  • RC. CHA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WAPYA, WAAHIDI KUFANYA KAZI KWA BIDII NA UADILIFU.

    July 01, 2025
  • TABORA: MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATAKIWA KUZINGATIA SHERIA NA MAADILI YA NCHI

    June 26, 2025
  • MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA YAENDESHA MAFUNZO MAALUM YA MATUMIZI YA MFUMO WA PEPMIS KWA WATUMISHI WA UMMA MKOA WA TABORA

    June 23, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa