HATIMAYE mifugo 462 ya mbolea yenye thamani ya shilingi milioni 55 ya Chama Kikuu cha Ushirika Milambo Ltd mkoani Tabora iliyokuwa imepotea katika mazingira ya kutatanisha na kumfanya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati kuagiza kukamatwa kwa Wajumbe wa Bodi na baadhi ya watendaji imepatikana.
Akizungunza wilayani Urambo kabla ya kukabidhi mifuko , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Safia Jongo alisema baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kutoa siku mbili kwa Polisi kuhakikisha wanapata mbolea yote walitumia kutumia mbinu mbalimbali za kuwabana baadhi ya watu waliokutwa na aina mbolea ambayo ilikuwa imepotea na hatimaye wamerejesha mifuko yote.
Alisema kuwa mbolea yote iliyopatikana imehifadhiwa katika Kituo cha Polisi Urambo wakisubiri kuikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa ili naye awakabidhi wahusika.
Dkt. Sengati akipokea mifuko hiyo alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanyakazi kwa haraka na kuhakikisha mifuko yote iliyokuwa imepotea inarudisha kwa ajili ya kupelekwa walengwa ili isaidie malengo ya kuendeleza zao la tumbaku mkaoni humo.
Alisema baada ya kupatikana mbolea yote hatua inafuata ni kuhakikisha mnyororo wote wa wahusika na upotevu huo unachukuliwa hatua nyingine kwa kuzingatia taratibu na kisheria ili kuondoa mzizi huo unaochafua ushirika Mkoani Tabora.
Dkt. Sengati alimwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora kuufuatilia mnyoyoro wote wa wizi wa pembejeo za wakulima ili kutoa somo kwa wengine wenye tabia hizo chafu na hatimaye kurudisha imani kwa wakulima na zao zima la tumbaku.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema muda wa kutaka kupata utajiri kwa njia ya rushwa, wizi, ubadhirifu na kuwanyonya wayonge umekwisha kinachotakiwa kila mtu afuate taratibu na sio njia za mkato kupata utajiri.
Dkt. Sengati alisema hawezi kukubali kuona kuwa baadhi ya watumishi, viongozi wa Ushirika, Benki na Kampuni waliopewa dhamana na Serikali wanashirikiana kuiba mali , pembejeo na fedha za wakulima.
Alisema wakulima wa tumbaku na mazao mengine ni lazima wanufaike na nguvu zao na wafurahie uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kutetea haki za wayonge.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa