NZEGA DC WAPEWA WIKI MBILI KUKABIDHI HOSPITALI KWA UONGOZI WA MJI WA NZEGA
MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amemwagiza Katibu Tawala Mkoa kuhakikisha ndani ya wiki ya mbili uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega unakabidhi Hospitali ya Wilaya kwa Halmashauri ya Mji wa Nzega.
Ametoa agizo hilo jana wakati wa Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani ya kupitia hoja ya mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/18.
Alisema tayari viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa walishaagiza kuwa Halmashauri ya Wilaya ikabidhi Hospitali kwa Mji wa Nzega.
“Hakuna haja ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kuendelea kung’ang’ania Hospitali kwani viongozi mbalimbali walishaagiza ikiabidhiwe kwa Mji wa Nzega kwa sababu ipo katika eneo lao” alisema.
Mwanri alisema hatua ya kukabidhi hiyo kwa Nzega Mji kutaisaidia Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kuomba fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali yake lakini ilivyo hivi sasa haiwezekani kupata fedha kwa kuwa bado inahesabika kuwa iko kwao.
Alisema inasikitisha kuona kuwa jambo hilo lishatolewa maamuzi na Viongozi wakuu lakini bado linajitokeza kwenye taarifa ya CAG na kuzalisha hoja ya kiukaguzi.
Mwanri alisema ndani ya mbili ni vema taratibu zote za maandalizi ya makabidhiano ziwe zimefanyika na usimamizi uanze kuwa wa Halmashauri ya Mji wa Nzega.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema itawachukulia hatua watumishi wote ambao watazisababishia Halmashauri kuzalisha hoja za kiukaguzi za kiukaguzi.
Alisema watumishi ambao wamepewa dhamana ya kukusanya mapato ya Serikali ni lazima wawe waaminifu katika kusimamia zoezi la ukusanyaji wa mapato kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa Wilaya husika na Taifa kwa ujumla.
Makungu aliwaomba Madiwani kuhakikisha wanafuatia utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Kata zao ili miradi hiyo iwe na ubora unaotakiwa.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Nzega William Jomanga alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa hatua ya kuingilia kati mvutano uliopo wa umiliki wa Hospitali ya Nzega.
Alisema hatua itawasaidia kuwa na usimamizi wa karibu na kuepuka kuzalisha hoja za kiukaguzi.
Mwisho
ReplyReply allForward |
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa