RAS TABORA AWATAKA WATUMISHI KUCHUKIA RUSHWA KWA VITENDO
KATIBU Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu amewataka watumishi Mkoani humo kuchukia rushwa kwa vitendo na sio kwa maneno ili waweze kutoa huduma kwa wananchi kwa uadilifu na haki.
Alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akifungua kikao cha siku moja cha watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega cha tathimini ya utendaji kazi wa Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Alisema uongozi wa Mkoa hauna mchezo na mtu yoyote atakayedhubutu kwa namna yoyote ili kushawishi rushwa kutoka kwa wananchi ili aweze kutoa huduma.
Makungu alisema vitendo vya rushwa kwa muda vimewahumiza wananchi wanyonge na nchi na kwa vingine vimechangia kuwarudisha nyuma kimaendeleo baada ya kukosa haki zao.
Alisema katika kupambana na rushwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imeshafanikisha kufungwa kwa mtumishi mmoja miaka mitatu kwa vitendo vyake vya kupokea rushwa.
“Tutaendelea kuwashughulikia bila huruma watumishi wote watakaodaiwa kudai rushwa …ni lazima watumishi wale mfano kwa waliochini yao katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwa wazalendo, waadilifu, waaminifu ili wananchi waweze kupata huduma wanayotarajia kuipata kutoka Serikalini” alisema.
Alisema mtumishi anayepokea rushwa sifa na haiba yake katika jamii inashuka na hakuna mtu anayeweza kumuheshimu.
MWISHO
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa