RC AAGIZA UCHUNGUZI WA NYARAKA ZA MALABI
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ally Hapi ameagiza viongozi wa sekta ya ardhi na vyombo vya usalama kukutana ndani ya wiki na Kamati ya Ursaimishaji na wananchi wanaodai kumiliki eneo la Malabi katika Manispaa ya Tabora kwa ajili ya kumaliza mgogoro uliodumu zaidi ya miaka 12.
Alisema ni lazima mkutano ufanyike kwa ajili ya kuwatambua wamiliki halali wa maeneo hayo kabla ya kuanza kwa kazi zoezi lilifanyika la urasimashaji ili haki iweze kutendeka kwa wahusika wote.
Hapi Hapi ametoa kauli hiyo jana wakati za ziara yake katika Manispaa ya Tabora ya kukatana na wananchi kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.
Alisema ikibainika kuwa walipewa viwanja katika maeneo hayo sio wahusika ni lazima hatua zichukuliwe za kuwaondoa na kuwapa kipaumbele cha kwanza katika ugawaji wa viwanja kwa wamiliki wa awali wa maeneo hilo.
Hapi alisema sanjari na hatua hiyo ameagiza Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kushirikiana na Polisi kufanyia uchunguzi nyaraka za urasimishaji eneo hilo ili ikibainika kuwa zimefanyiwa mchezo mchafu wahusika weze kuchukuliwa hatua.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema Kamati iliyoundwa kurasimisha eneo ambao awali lilikuwa likimilikiwa na Serikali walitoa viwanja kwa watu wengi na kuwaacha wamiliki bila maeneo ya kujenga makazi.
Walisema baadhi ya viongozi wa Kamati ya Urasimishaji walidiriki hata kughushi mitahasari ya vikao kwa ajili ya kuficha ukweli wa umuliki wa eneo hilo ili kujipatia fedha kwa njia ya dhuluma.
MWISHO
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa