RC ATAWAKA WAKAZI WA TABORA KUCHAPA KAZI BAADA YA KUMALIZIKA ZOEZI LA KUWACHAGUA VIONGOZI
BAADA ya kumalizika zoezi la kupiga kura na kutangazwa washindi wakazi wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kuendelea na shughuli zao mbalimbali za kila siku za kujitafutia maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na MKuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati kwenye mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake.
“Uchaguzi umefanyika kwa amani na utulivu na wananchi wamepokea matokeo kwa utulivu wa hali ya juu ... hakuna matukio yaliyojitokeza ambayo yaliashiria uvunjifu wa amani kuanzia wakati wa kampeni hadi siku ya uchaguzi…tunawashukuru sana wananchi kwa utulivu huo ”alisema
Dkt. Sengati alisema baada ya mchakato wa kidemokrasia kumalizika , wananchi wanatakiwa kuchapakazi kwa bidii kwa ajili ya ustawi wa Mkoa wa Tabora na Taifa zima.
Aliongeza kazi zilizosalia ambazo zinahusu masuala ya uchaguzi ziachiwe kwa Mamlaka ambayo imepewa dhamana ya kusimamia uchaguzi.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi wakati wa Kampeni na siku ya kutimiza haki ya kidemokrasi ya kuwachagua viongozi wanaowapenda.
Mwisho
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa