MKUU wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati ametoa siku 38 kwa uongozi wa Mamlaka ya Elimu na Ufundi (VETA) kukamilisha ujenzi wa miradi miwili ya vyuo vya Igunga na Uyui ili ianze kutoa mafunzo kwa wakazi wa maeneo hayo.
Miradi hiyo inajengwa kwa niaba ya VETA na Chuo cha Ufundi Stadi Tabora kwa upande wa Wilaya ya Uyui na Chuo cha Ufundi Stadi Shinyanga kinajenga cha Igunga kwa niaba ya VETA imeshindwa kukamilika katika vipindi viwili walivyoongezewa nje ya kile cha awali cha Juni mwaka huu.
Dkt. Sengati alitoa kauli na baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya Vyuo vya Ufundi Stadi Uyui na Igunga na kukuta kazi bado haijakamilika licha muda waliongezewa kubaki siku chache.
Alisema awali ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi Uyui na Igunga vinavyojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 1.5 kwa kila kimoja ukamilikea Juni baadae wakaongezewa hadi Agosti na baada ya hapo wakaongeza hadi Desemba mwaka huu na bado dalili haionyeshia kama watakamisha mwisho mwa mwezi huu.Dkt. Sengati alisema ifikapo tarehe ya 31 Januari hapo mwakani ni lazima ujenzi wa vyuo vyote uwe umekakamilika kwa asilimia mia moja na vianze kudahili wanachuo.
Alisema hakuna sababu ya uongozi wa Vyuo vyote vilivyopewa jukumu la kusimamia ujenzi kuchelewesha kwa kuwa walishapewa fedha na Serikali na vifaa vinavyohitajika vipo.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema sababu za kuchelewa kwa miradi ikiwemo kudai mvua na kufuata kokoto mbali hazina nguvu wanachotakiwa ni kuchapakazi usiku na mchana ili miradi ikamike hapo Januari mwakani.
Alisema lengo ni kutaka watoto waliomaliza elimu ya msingi na kukosa fursa ya kuendelea na masomo ya Sekondari waweze kudahiliwa vyuo hapo kwa ajili ya kusoma fani mbalimbali za ufundi ambazo zitawasaidia kushiriki vema katika ujenzi wa Taifa.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Mafundi wanaoshiriki ujenzi wa Vyuo hivyo kutoa fursa za ajira kwa vijana waliopo karibu na maeneo ya miradi ili mzunguko wa fedha kwa wakazi hao uwe mkubwa.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA )Kanda ya Magharibi Wilhard Soko alimweleza Mkuu wa Mkoa wa Tabora watajitahidi kuwasimamia vyuo vya Tabora na Shinyanga ili vikamilishe miradi yote miwili kama waliahidi kukamilisha Mwezi Januari mwakani.
Alisema baada ya kukamilika ujenzi hatua zinafuata za ununuzi wa vifaa ufanyike na waweze kudahili wanachuo kwa ajili ya kuanza masomo.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa