RC TABORA AAGIZA KUUNDA KAMATI YA KUCHUNGUZA MGOGORO KATIKA MRADI WA UMWAGILIAJI WA INALA KATIKA MANISPAA YA TABORA
MKUU wa Tabora Dkt. Philemon Sengati amemwagiza Katibu Tawala Mkoa kuundwa kwa Kamati ya kuchunguza mgogoro unaoendelea kwenye mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika bwawa la Inala lilipo Manispaa ya Tabora ambao umekuwa ukitishia amani.
Alitoa agizo hilo mjini Tabora baada ya kutembelea mradi huo kwa lengo la kusikiliza kero ya wakulima wa eneo hilo ili kuzitafutia ufumbuzi.
Dkt. Sengati alisema Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 1 katika mradi huo wa mwagiliaji wa Inala kwa lengo la kutaka kuondoa upungufu wa chakula katika Manispaa ya Tabora badala yake kumekuwepo kwa migogoro ambayo inakwamisha uzalishaji.
Alisema migogoro hiyo imesababishwa na baadhi ya watu wachache wakiwemo viongozi ambao wameweka maslahi binafsi kwa kutaa maeneo ya wananchi.
Dkt. Sengati alisema uongozi wa Mkoa hauwezi kuona kuwa mradi huo wa kimkati ufie mikononi mwao bila kuchukua hatu.
Alisema Kamati hiyo inatakiwa ichunguze kiini cha mgogoro na kutoa mapendekezo ya kuumaliza ndani ya siku saba ili wakulima wa eneo hilo waendelee kufanya kazi zao kwa amani kwa ajili ya kuzalisha mazao mengi ili kuwa na uhakika wa usalama wa chakula.
Dkt. Sengati alisema Kamati hiyo inatakiwa kuwa na wanasheria kutoka Ofisi yake, Watalaamu kutoka Umwagiliaji na wabobezi wengi ambao watasaidia kutoa mwelekeo kwa kumaliza mgogoro huo.
Aliongeza kamati hiyo ni lazima ifanyie uchunguzi wa maeneo ya wananchi yaliyochukuliwa bila kufuata utaratibu ikiwemo yale ambayo Baraza la Madiwani lililoagiza yachukuliwe bila kuwahusisha wahusika.
Aidha Mkuu wa Mkoa aliwataka viongozi waliopewa jukumu la kuendesha mradi huo kusimamia haki na kuwawezesha wakulima wa eneo hilo kuzalisha kwa wingi.
Alisema Serikali haitasita kuwachukulia hatua watumishi na viongozi ambao wamechukua maeneo ya wakulima hao bila kufuata utaratibu unaongoza mradi kwa lengo la kuwanyanyasa wakulima.
MWISHO
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa