WANANCHI wilayani Kaliua ambao wamevamia maeneo ya hifadhi za mistu wametakiwa kuondoka haraka na kuacha kuendesha shughuli zozote ndani ya maeneo hayo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Kaliua.
Alisema ni kinyume cha Sheria kwa watu kuishi na kufanya shughuli zozote za kiuchumi katika maeneo yote ya hifadhi na watakaokutwa humo watachukuliwa hatua kali.
“Ninajua wapo watu kwenye hifadhi …watu hao hawapendi Amani …tutakaowakuta katika maeneo hayo tutakabiliana nao ipaswayo…maelekezo ni kwamba maeneo ya hifadhi harusiwi mtu au kikundi chochote kufanya shughuli za uchumi” alisisitiza
Dkt. Sengati aliwataka wau kufanyakazi katika maeneo rasmi na sio yale ambayo yamezuiliwa kisheria kwa ajili ya manufaa ya Taifa zima.
Mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa wananchi wenye mapenzi mema na ustawi nchi kuwafichua watu wote ambao wamekuwa wakiingia katika maeneo ya hifadhi na kufanya uharibifu ili hatua kali dhidi yao ziweza kuchukuliwa.
Alisema Serikali haiwezi kuvumilia kuona watu wanaingia katika maeneo hayo na kuhatarisha usalama wa wananchi wengine na kuhatarisha vyanzo vya maji na viumbe hai wengine.
Dkt. Sengati aliiagiza Kamati ya Usalama Wilaya kushirikiana na uongozi wa Halmashauri na jamii zinazozunguka Hifadhi hizo ili kuwaondoa wavamizi na kuzuia wengine wasiweze kuingia kwa ajili ya kuendesha shughuli ambazo haziruhusiwi.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora amesema kuwa endapo itabainika kuwa kuna baadhi ya watumishi na viongozi wanashiriki katika kuchochea tabia hiyo ya wananchi kuvamia maeneo ya hifadhi watachukuliwa hatua kali.
Alisema kuwa wapo watumishi na viongozi wa aina hiyo ni vema wakaacha mara moja kabla hawachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya Sheria.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaliua Simon Nyahinga alisema wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la vikundi vya watu kuingia katika maeneo ya Hifadhi za Mistu na kuendesha shughuli mbalimbali za kilimo na ufugaji.
Aliongeza kuwa watu hao wamekuwa wakati mwingine wakiwashambulia ,kuwadhuru , na kuwaua watendaji wanaojaribu kutaka kuwaondoa.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa