RC TABORA AMWAGIZA RAS KUPELEKA WAUGUZI KATIKA ZAHANATI YA CHAMPERA WILAYANI IGUNGA
KATIBU Tawala Mkoa (RAS) Mkoani Tabora ameagizwa kuhakikisha anapeleka watumishi wa sekta ya afya katika Zahanati Chapera wilayani Igunga ili ianze mara moja kutoa huduma za matibabu kwa wakazi wa eneo hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wilayani Igunga wakati wa Baraza maalumu la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo la kujadili hoja mbalimbali za Mkaguzi wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka huu.
Alisema wakati Mkoa ukisubiri ajira za watumishi wapya ni vema Katibu Tawala Mkoa kuangalia uwezekano wa kuwagawanya watumishi waliopo kazi katika Zahanati ya Champera na maeneo ambayo hayana watumishi ili wananchi wa maeneo hayo nao waweze kupata huduma za afya karibu na mazingira yao.
Mwanri alisema hoja ya Mkaguzi wa Nje ni vema ikatatuliwa kwa kugawanya watumishi waliopo katika vingine katika maeneo yasiyokuwa na watumishi kabisa.
Katika hatua nyingine Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga imeagizwa kuhakikisha inakusanya deni la shilingi milioni 42.4 kutoka kwa wananchi ambao hajawalipia viwanja walivyouziwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alitoa hoja hiyo na kuungwa mkono la Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kufuatia hoja ya Kamati ya Ukaguzi kutoka Ofisi ya Mkaguzi wa Nje baada ya kubaini deni hilo.
Alisema kiasi cha deni hilo ni lazima kikuswanywe na hatua zichukuliwe ikiwa ni pamoja na wahusika kupewa mwezi mmoja ili walipe madeni yao na wakishindwa viwanja hivyo virejeshwe katika Halmashauri.
Mwanri alisema baada ya Mwezi mmoja kuisha wahusika ambao wameshindwa kulipia vijanywa wanyang’anywe na viuzwe kwa wengine ili kulipa deni hilo.
Kwa upande wa Mkaguzi wa Nje kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mku wa Hesabu za serikali (CAG) Erasto Juma alisema jumla ya mapato ya shilingi milioni 42.4 yaliyotokana na mauzo ya viwanja kwa wanunuzi 76 katika maeneo ya Nkokoto hayakuweza kukusanywa.
Alisema ni kiasi cha milioni 4 tu ndizo zilizokusanywa na kusalia kwa deni hilo.
Halmashauri ya wilaya ya Igunga katika ukaguzi wa Hesabu unaoishia Juni 30 imepata hati inayoridhisha.
MWISHO.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa