RC TABORA ASEMA UBORESHAJI WA UWANJA WA NDEGE WA RESOLUTE WILAYANI NZEGA KWA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA
Mkuu wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema upanuaji na uboreshaji wa Uwanja wa Ndege wa Resolute wilayani Nzega utakuwa ni muhimu kwa maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda.
Amesema kuwa Uwanja huo utawawezesha wataalamu na Wafanyabiashara kufikia eneo kwa urahisi na kwa kutumia muda mfupi.
Balozi Dkt. Batilda amesema hayo leo wakati akizungumza na Timu ya Wizara ya Ujenzi na uchukuzi ambayo ilitumwa kuangalia uwezekano wa kupanua Uwanja wa Ndege wa Resolute wilayani Nzega kwa ajili ya kuruhusu Ndege za Biashara kuruka na kutua kupitia Uwanja huo.
Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ilibaini kuwa Uwanja huo unaweza kupanuliwa kwa kuwa lipo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 1,000 ambalo linafaa kwa Uwanja utakaowezesha ndege za biashara kufanya safari zake.
MWISHO
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa