WAZAZI wenye watoto katika Shule za Msingi na sekondari Mkoani Tabora wameshauriwa kuangalia uwezekano kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao.
Hatua itawasaidia kuongeza usikivu darasani na hatimaye kufanya vizuri katika masomo yao.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Nzega ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya shule.
Alisema watoto wanaoshinda njaa wanakuwa na usikivu hafifu darasani hasa katika vipindi ambavyo vinafundishwa saa za mchana na kuwafanya vibaya katika masomo yao.
Dkt. Sengati alisema kuwa kitendo cha watoto kuwa na uhakika wa kupata chakula shule kinachangia kuondoa utoro na kuongeza mahudhurio ya wanafunzi shuleni.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema jambo la msingi ni wazazi kukutana na kukubaliana njia nzuri na utaratibu unakubalika kwa wao kuchangia chakula ili kuepusha malalamiko.
Alisema chakula watakachongia ni kile ambacho watoto wao wangekitumia kama wangekuwa nyumbani
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa