MKUU wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati amewataka watumishi wa umma kuondoka Ofisini na kwenda kwa wananchi kusikiliza na kutatua kero zao.
Alitoa agizo hilo wakati wa mkutano wa hadhara Wilayani Nzega baada ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya shule.
Dkt. Sengati alisema ni marufuku kwa Watumishi wa umma kuwangonja wananchi wawafuate ili kuelezea shinda na matatizo yao bali ni jukumu la watumishi kwenda kwa wananchi.
“Watumishi msikae kwenye viyoyozi na viti vya kuzunguka…nendeni kwa wananchi mkawasilize kisha mtatue matatizo mbalimbali yanayokabili katika kujiletea maendeleo” alisema.
Alisema wananchi ndio waajiri wa watumishi wanapaswa kuhudumiwa kwa mujibu sheria ili kutimiza matarajio ya huduma wanaitaka kutoka kwa Serikali.
Dkt. Sengati alisema watumishi wanatakiwa kufanya kazi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli alivyotoa kuwatumika wananchi wanyonge ili nao wafaidi matunda ya nchi yao.
Aliongeza kuwa ni jukumu la kila mtumishi katika eneo lake kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata haki na wanakuwa na mazingira mazuri ya kushiriki shughuli za maendeleo.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa