RC TABORA AWATAKA WATAALAMU KUSAIDIA WALENGWA WA TASAF KUTUMIA FEDHA ZAO KUIBUA MIRADI
MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewaagiza Wataalamu kusaidia katika utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya fedha wanazopatiwa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini(TASAF) ili waweze kuanzisha miradi itakatowaendeleza wenyewe.
Aliota kauli hiyo jana wakati wa Kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF na kutoa mwongozo wa utambuzi na uandikishaji wa kaya za walengwa katika eneo la Utekelezaji kwenye Manispaa ya Tabora.
Alisema fedha wanazopata walengwa wanaweza kuzitumia katika shughuli mbalimbali ikiwemo ufugaji wa nyuki, kuku na mifugo mingine ambayo itawakomoa na kuwafanya wapande daraja na kuacha kutegemea ruzuku ya Serikali.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kupitia TASAF kaya zaidi milioni 1 zimenufaika na kufanyakazi za ujasiriamali na kuweza kuendesha maisha yao kwa unafuu ukilinganisha na awali.
Balozi Dkt. Batilda alisema Mkoa wa Tabora unazofursa nyingi kama vile mistu mikubwa , ardhi ya kutoa na mifugo mingi ambapo walengwa wanaweza nao kutumia nafasi hizo kusonga mbele kimaisha.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa aliagiza kufungwa kwa Kamera za ulinzi(CCTV Camera ) katika maeneo makubwa ya biashara ikiwemo minadani masokoni ili kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali.
Alisema sanjari na hilo ni vema Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ikaimarishwa ili kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Balozi Dkt. Batilda alisema alisema katika maeneo ambayo yamefungwa mifumo ya TEHAMA imeonyesha mafanikio makubwa ambapo mapato ya Serikali yapanda mara tatu ya awali.
Awali Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) Gerald Macha alisema utambuzi wa awamu utafanywa kwa makini na wahusika watakula kiapo ili kuepuka kuingiza majina ya watu wasiostahi
MWISHO
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa