SERIKALI za Mkoa wa Tabora imezitaka Halmashauri za Wilaya kuweka kiasi cha shilingi 1,000/= za lishe katika bajeti zao kulingana na idadi ya watoto waliochini ya miaka mitano katika maeneo yao.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora ,Dkt. Philemon Sengati wakati akifungua kikao cha siku moja cha tathimini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa ngazi ya Mkoa.
Alisema pia kila Halmashauri ya Wilaya ni lazima itenge chumba katika Kituo cha Afya na Hospitali cha kutibia watoto wenye utapiamlo mkali na kutenga fedha za kununulia mahitaji ya kutengeneza vyakula lishe kwa matibabu ya watoto wenye utapiamlo mkali.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora , Dkt. Sengati amezitaka Halmashauri za Wilaya ambazo hazifanya kikao cha tathimini ya mkataba wa lishe kujieleza kwa kushindwa kujadili katika ngazi ya Kata na Kijiji.
Alisema ni Halmashauri ya Wilaya ya Igunga pekee kati ya nane ndio imetekeleza kikao cha tathimini ya mkataba wa lishe ambacho ni muhimu cha kujadili matatizo yanayokabili afua za lishe na kutafuta ufumbuzi wake.
Dkt. Sengati alisema vikao hivyo ni muhimu kwa kuwa vitasaidia kugundua matatizo mapema na kuchukua hatua kabla ya athari hazijawa kubwa.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa taarifa za takwimu za kutoka Julai hadi Desemba mwaka jana Halmashauri sita hazikufanya vizuri kwenye kiashiria cha matibabu ya utapiamlo kwa watoto wa chini ya miaka mitano.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa