Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema wanatarajia kutengeza mizinga ya kisasa laki mbili (200,000) kwa mwaka huu ili kuongeza uzalishaji wa asali.
Alisema mpango huo unatarajiwa kufanyika baada ya mkutano na wadau wa sekta ya ufugaji na uzalishaji wa asali kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kutoa mafunzo ya utengezaja wa mizinga ya kisasa.
Balozi Dkt. Batilda amesema hayo leo Ofisi kwake alipokutana na Wajumbe wa Kamati iliyoundwa na Wizara ya Maliasili na Utalii ya kufuatilia Malalamiko ya Mwingiliano wa Matumizi ya Ardhi katika Mapori yaliyopandishwa Mkoani Tabora.
Amesema hivi sasa Mkoa wa Tabora una mizinga ya asali 407,688 na kisasa 43,143 ambayo ina uwezo wa kuzalisha kuzalisha tabi 2,437 za asali na nta tani 90.
Balozi Dkt. Batilda amesema wanataka kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ya nyuki kwa ajili ya kuwainua kiuchumi wafugaji na kuutangaza Mkoa wa Tabora dunia kote kwa ufugaji wa nyuki.
Amesema watatumia Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki Tabora kutoa mafunzo kwa vijana wengi kuhusu utengezaji wa mizinga ya kisasa ili waunde vikundi ambavyo Halmashauri za Wilaya kupitia mikopo ya asilimia 10 itaviwezesha kuanzisha maeneo makubwa ya ufugaji kwa ajili ya kuongeza wingi asali.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema sanjari hilo la kutoa mafunzo ya ufugaji wa nyuki watakitumia Chuo hicho kuzalisha makundi ya nyuki ambayo yatatolewa kwa wafugaji ili waongeze uzalishaji.
Aidha Balozi Dkt. Batilda amesema wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kuepuka ucomaji moto na kuendesha kilimo ambacho kinazingatia utunzaji wa mazingira kwa ajili ya kuwa na maeneo ambayo yataachwa ili kufugaji nyuki.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza Wajumbe wa Kamati iliyoundwa na Wizara ya Maliasili na Utalii ya kufuatilia Malalamiko ya Mwingiliano wa Matumizi ya Ardhi katika Mapori yaliyopandishwa Mkoani Tabora kutoa na mapendekezo ambayo yatasaidia kuondoa migogoro baina ya wananchi na Mamlaka ya Uhifadhi wa Wanyamapori (TAWA) na Wakala wa Uhifadhi wa Mistu Nchini (TFS).
Amesema mapendelekezo ni vema yakalenga kuendeleza uhifadhi endelevu na matumizi ya maendeleo ya wananchi bila kuathiri uhifadhi.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa