TABORA YAKUSANYA BILIONI 13.5 TOKA MAPATO YA NDANI TOKA JULAI HADI MACHI
JUMLA ya shilingi bilioni 13.5 zimekusanywa na Halmashauri za Mkoa wa Tabora katika kipindi cha Julai hadi Machi mwaka huu.
Fedha hizo zimetokana na makusanyo yanayotokana na mapato ya ndani ambayo ni sawa na asilimia 51.9 ya lengo la kukusanya bilioni 24.1.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua.
Alisema kiasi hicho cha makusanyo hakiridhishi kwa kuwa bado kuna Halmashauri ambayo hazijafika hata asilimia 50 na bado miezi mitatu mwaka wa fedha umalizike.
Makungu alisema Halmashauri ya Wilaya ya igunga ndio inaoongoza kwa kufiksha asilimia 70 ambapo imekusanya shilingi bilioni 1.9 kati ya bilioni 2.7 na Uyui imekusanya bilioni 1.6 ambayo ni asilimai 67 kati ya bilioni 2.5.
Alisema kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua imekuusanya bilioni 2.4 sawa na asilimia 64 ya shilingi bilioni 3.6, Sikonge imekusanya shilingi bilioni 1.7 sawa na asilimia 61 ya shilingi bilioni 2.8 na Nzega Mji imekusanya bilioni 1.2 sawa na asilimia 61 ya bilioni 2.
Katibu Tawala huyo wa Mkoa alisema Manispaa ya Tabora imekusanya shilingi bilioni 2.3 ikiwa ni asilimia 50 ya makisio ya shilingi bilioni 4.6, Urambo imekusanya bilioni 1.3 sawa na asilimia 44 ya bilioni 3 na Halmashauri ya Wilya ya Nzega imekusanya milioni 907.8 sawa na asilimia 35 ya bilioni 2.6.
Aidha ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa watumishi wa Halmashauri zote waliopewa mashine za kukusanyia mapato (POS) ambao wamekusanya mapato na kushindwa kuyawasilisha Benki.
Makungu alisema kuanzia sasa ni marufuku kutumia fedha zinazokusanywa na Halmashauri kabla hazijapelekwa benki kwa kuwa vitendo hivyo ndio vinavyosababisha hoja za CAG.
Alisema ni lazima hatua za makusudi zichukuliwe kuondoa dosari zinazozalisha hoja ikiwemo kujibu hoja na kuepusha kuwa sehemu ya kuzalisha mpya.
Mwisho
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa