MKUU wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati amewataka Vijana walioajiria katika sekta mbalimbali za umma kuhakikisha wanafanyakazi kwa bidii na kwa kuzingatia misingi ya uadilifu na uzalendo.
Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Kaliua.
Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameonyesha imani kubwa kwao na kutoa fursa nyingi za ajira kwao kushika nyadhifa mbalimbali , hivyo ni vema wakatumia fursa hiyo kuchapakazi kwa bidii.
“Kipindi hiki vijana wamepata fursa nyingi ni vema mkamuonyesha Rais kuwa hakukosea kuwateua na kuwapata nafasi mbalimbali kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania kuondokana na umaskini” alisema.
Dkt. Sengati aliwataka vijana kuachana na tamaa za kutaka utajiri wa haraka kwa kuwa utawasababisha kupoteza mwelekeo wa maisha yao na wasifu wao( CV).
Alisema kuwa vijana bado wanayosafari ndefu ni vema wakahakikisha wanazingatia maadili ya utumishi wa umma na kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria, taratibu na Kanuni ili waweze kuheshimika na hatimaye kuendelea kupata madaraka makubwa.
Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Watumishi wa umma kufanyakazi kama timu moja na kuwa wabunifu wakati wote wawapo kazini ili waweze kuwasaidia wananchi wanyonge kupata haki zao na kuondokana na umaskini.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa