VIJIJI VYOTE VYA MRADI WA REA KUWA NA UMEME IFAKAPO DESEMA MWAKA HUU: DKT KALEMANI
SERIKALI imetoa miezi mitatu kwa Wakandarasi wanaotekeleza mradi wa kabambe wa kusambaza umeme vijijini nchini awamu ya tatu (REA III) kuhakikisha wamekamilisha kuunganisha umeme katika vijiji vyote vilivyopo katika mradi huo ifikapo Desemba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani wakati wa uzinduzi wa kuwasha umeme katika eneo la Mwambaha wilayani Nzega.
Alisema endapo itafika Desemba mwaka huu kazi haijakamilika itabidi Serikali ichukue hatua dhidi ya Mandarasi ambaye atakuwa hajaunganisha umeme katika Vijiji walivyokubaliana.
“Kwa vile Sasa hakuna changamoto ya vifaa kama vile nyaya, nguzo na transformer , ni matarajio yetu speed itakuwa kubwa na kuunganisha umeme katika vijiji mbalimbali…kwa hiyo tusingependa kuona Mkandarasi anakuwa mzembe kwa hatua yoyote ile…tukiona mkandarasi akuwa mzembe ni vema tuone ni hatuna gani tunachukua mapema badala ya kusubiri hadi mwisho” alisisitiza.
Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha vijiji vyote vilivyo katika REA III vinafikiwa umeme , kazi itakayobaki ni kusambaza kwa mwananchi mmoja mmoja anayelipia umeme .
Aidha Dkt. Kalemani alisema Serikali imeagiza katika maeneo ambayo njia kuu za umeme zinapita na vitongoji na vijiji ambavyo havina umeme ,Shirika la Ugavi wa Umeme nchini(TANESCO) kuhakikisha navyo vinapata umeme.
Katika hatua nyingine Serikali imetoa shilingi bilioni 2.5 kila Mkoa ili kuimarisha miundombinu ya usambazaji umeme nchini.
Dkt. Kalemani alisema fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa nguzo, nyaya na ‘transformer’ ili kuzuia kukatikati kwa umeme mara kwa mara hapa nchini na kusaidia wananchi kuwa na fursa za kufungua njia kubwa za uchumi na ujenzi wa viwanda.
Wakati huo huo Waziri wa Nishati amewataka wananchi ambapo umeme tayari umefika kuchangamia fursa za mradi wa REA III ili waweze kuunganisha umeme ili uwasidie kuanzisha viwanda vidogo vidogo ikiwemo vya kusindika mazao kwa ajili ya kuyaongezea ubora.
Alisema upatikanaji wa umeme utawasaidia kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kiusalama na hivyo ni vema wakachangamkia fursa hiyo iliyotolewa na Serikali.
Mwisho
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa