WATUMISHI TEKELEZENI MIRADI KWA UADILIFU KULIPA FADHILA KWA RAIS MAGUFULI –KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU
WATUMISHI wa Umma wametakiwa kulipa fadhila kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa kufanyakazi kwa kuzingatia taraibu na Sheria wakati wa utekelezaji wa miradi wanayokuwa wamepewa kusimamia.
Kauli hiyo imetolewa leo na Kiongozi wa Taifa Mbio za Mwenge wa uhuru Mzee Mkongea Ali ikiwa ni siku ya pili za mbio zake Mkoani Tabora kwenye Halmashauri ya Mji Nzega baada ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imetoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi ikiwemo ujenzi wa Hospitali za Wilaya, vituo vya Afya , usambazaji wa maji na barabara , hivyo ni vema miradi hiyo ilingaline na thamani ya fedha zilizotolewa.
Ali alisema hatua hiyo itasaidia kuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki sawa kama yalivyo malengo ya Rais ya kuhakikisha watanzania wote wanafaidi rasilimali za nchi kwa kupata huduma zote muhimu ikiwemo elimu na afya.
Kiongozi huyo akiwa katika Halmashauri ya Nzega Mji ameweka mawe ya msingi miradi ya maendeleo minne ikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5.
Miradi hiyo ni ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Nzega Mji na mradi wa ujenzi wa Mji wa Kisasa wa Ipazi katika eneo la Kitangile , ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwenye Msikiti wa Ijumaa na Kituo cha Afya cha Cithian
Katika hatua nyingine Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ali ametoa mwezi Mmoja kwa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini(TARURA) katika Halmashauri ya Nzega Mji na Mkandarasi M/S Mgalang’ombe kufanyia marekebisho maunganisho ya Msikiti Mkuu wa Ijumaa na ile inayotoka katika maegesho ya malori.
Alisema marekebisho ni pamoja na kuondoa mgongo unaonyesha barabara zilizopounganisha na kuifanya isiwe na muonekano mzuri.
Mwisho
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa