WATUMISHI WA MANISPAA YA TABORA WANAODAIWA KUANZA KUKATA FEDHA KATIKA MISHAHARA
MENEJIMENTI ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imepewa wiki moja kuhakikisha inaanza kuwakata katika mishahara watumishi wote ambao wanaodaiwa masurufi yaliyosababisha kufikia shilingi milioni 4.7 ambayo yamesababisha kuzalishwa kwa hoja ya kiukaguzi.
Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani ya kupitia hoja ya mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2017/18.
Alisema ndani ya wiki watumishi wote wanaodaiwa wahakikishe wamelipa fedha hizo au wakatwe kwenye mishahara yao.
Mwanri alisema wasipo katwa fedha hizo hoja hiyo itaendelea kujitokeza na kuchafua hesabu za Manispaa ya Tabora.
Sanjari na hilo Mkuu wa Mkoa huyo ameetoa wiki mbilli kwa Wakuu wa Idara kuhakikisha wamefanyia kazi hoja zote za CAG na kuwalisilisha vielelezo ili ziweze kufungwa .
Alisema Mkuu wa Idara ambaye ndani ya kipindi hicho hatashindwa kujibu hoja hizo na kusababisha kuendelea kuwepo atachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuondolewa katika nafasi yake.
Mwanri alisema hoja zigawanywe katika Wakuu wa Idara mbalimbali ili waanze kuzifanyika kazi mapema.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora imewataka uongozi wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanakusanya madeni yote ya ardhi na mikopo ya wanawake, vijana na walemavu zaidi ya milioni 536.
Alisema eneo la kwanza linatokana na mauzo viwanja ambapo waliotakiwa kufidiwa maeneo yao hawakulipwa na wale ambao walipewa viwanja wamekuwa wakilipa kidogo dogo na kusababisha deni kufikia milioni 503.
Mwanri alisema ni vema wakakaa chini na kushughulikia tatizo hilo ili hoja hiyo iweze kufutwa na kuondolewa katika vitabu vya CAG.
Kwa upande wa mikopo iliyotolewa kwa vikundi vya wanawake na vijana ipatayo shilingi milioni 33.7 ambayo haijarejeshwa.
Alisema ni vema fedha hizo vikundi hivyo vifuatiliwe na virudishe mikopo hiyo kwa ajili ya kutoa katika vikundi vingine.
Aidha Mkuu huyo Mkoa amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora kuonyesha mpango wa kulipa madeni mbalimbali ambayo wanadaiwa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora Komanya Kitwala alimtaka Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa kuwachukulia hatua watumishi wote ambao wameisababishia Halmashauri hiyo kuzalisha hoja za kiukaguzi.
Alisema watumishi ni vema wakajitahidi kuzuia hoja na zio kutoa maamuzi ambayo yanasababisha kuendelea kuzalisha hoja kila mwaka .
Mwisho
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa