USIMAMIZI WA UTOAJI WA LESENI ZA BIASHARA KWA MKOA WA TABORA
Mamlaka za utoaji wa leseni za biashara za kundi ‘B’ zinatoa leseni hizi kwa uwazi kwa kuweka taratibu zinazotakiwa kutimizwa na waombaji na kiasi cha ada wanachotakiwa kulipa kulingana na biashara wanazoomba kwenye tovuti zao na mbao za matangazo ili wanachi wajue kiasi wanachopaswa kulipa na taratibu za kufuata ili kupata leseni. Aidha, malipo yote ya ada za leseni hulipwa kupitia Benki na hivyo kuondoa mwanya wa uvujaji wa mapato ya Serikali. Mwelekeo wa sasa ni kuanza kutoa leseni kwa njia za kieletroniki ili kurahisisha huduma hiyo. Kwa leseni za kundi ‘A’ BRELA wapo katika hatua za mwisho za maandalizi ya utoaji leseni kielertoniki.
Mkoa umekuwa ukisimamia Sheria ya Leseni ya Mwaka 1972 kwa kuzihamashisha halmashauri kuwarasimisha wafanyabiashara wake kwa kuwapatia leseni ambazo zitaongeza mapato na pia Mkoa umekuwa ukifanya ukaguzi wa hali ya utekelezaji wa Sheria ya leseni. Mamlaka za serikali za Mitaa zimekuwa zikihamasisha wafanyabiashara kuteleleza Sheria ya Leseni za biashara na zimekuwa zikitoa leseni mbalimbali za biashara kwa wafanyabiashara. Jumla ya Vitabu vya Leseni ya Biashara 107 vimetumika kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na kukusanya jumla ya Tsh.1,139,326,650 katika Mkoa wa Tabora. Vitabu vya leseni 18 vinaendelea kutumika hadi ifikapo tarehe 30/06/2022
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa