Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Gelasius Byakanwa ametembelea wajasiriamali kutoka Mkoa wa Tabora ambao wameshiriki kwenye maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika mjini Bujumbura, Burundi
Kwa Mwaka huu Wajasiriamali zaidi ya arobaini (40) kutoka kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Tabora wameshiriki kwenye maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika mjini Bujumbura, Burundi kuanzia Disemba 5, 2023 hadi Disemba 15, 2023. Kauli mbiu inasema “Kuunganisha Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki kufanya biashara katika eneo la Jumuiya ya Afrika Mashariki”.
Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Gelasius Byakanwa akiwa kwenye maongezi na baadhi ya wawakilishi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Cercle Hyppique (Golf Course) vilivyopo mjini Bujumbura, Burundi kabla ya kwenda kuwatembelea wajasiriamali kutoka Mikoa Tanzania walioshiriki kwenye maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika mjini Bujumbura, Burundi kuanzia Disemba 5, 2023 hadi Disemba 15, 2023.
Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Gelasius Byakanwa akitembelea mmoja wa wajasiriamali kutoka Mkoani Tabora walioshiriki kwenye maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika mjini Bujumbura, Burundi kuanzia Disemba 5, 2023 hadi Disemba 15, 2023.
Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Gelasius Byakanwa akipata elimu kuhusiana na Asali ya Tabora kutoka kwa mmoja wa Wajasiriamali walioshiriki kwenye maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika mjini Bujumbura, Burundi kuanzia Disemba 5, 2023 hadi Disemba 15, 2023.
Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Gelasius Byakanwa akipata elimu kuhusiana na faida za unga wa gogondi kutoka Tabora kutoka kwa mmoja wa Wajasiriamali walioshiriki kwenye maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika mjini Bujumbura, Burundi kuanzia Disemba 5, 2023 hadi Disemba 15, 2023.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa