Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt Batilda Burian amefanya halfa ya kufunga mwaka iliyofanyika kwenye ukumbi wa mkutano uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora. Ambapo kwenye hafla hiyo iliyo wakutanisha watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, viongozi wa Dini na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa.
Katika halfa hiyo Dkt Batilda Burian alipata nafasi ya kuzungumza na waalikwa ambapo kwenye hotuba yake alisisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa Umma kwa kuzingatia maadili.
Sambamba na hilo Dkt Batilda alipata nafasi ya kumushukuru Mh.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwakuleta miradi mbalimbali ikiwemo hospitali kila Wilaya, ujenzi wa bomba la mafuta obereshajwi wa huduma ya afya, ukuaji wa sekta ya kilimo, usambazaji wa maji, ujenzi wa madarasa pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa yaani SGR. Na kwamba ukamilishwaji w miradi hiyo ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinfuzi (CCM)
Aidha Dkt Batilda ameishukuru kamati ya ulinzi na Usalama (M) Tabora pamoja na zile kamati za ulinzi na Usalama za Wilaya na kusisitiza kuwa Mkoa wa Tabora Upo Salama hasa katika kipindi hiki cha Sikukuu.
Kwenye hotuba yake Dkt Batilda amewashukuru watumishi wote wa Mkoa wa Tabora kwa kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo na kusisitiza uwajibikaji.
Kwa upande mwingine amewataka wananchi wa Mkoa wa Tabora kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye miradi inayotekelezwa Mkoani Tabora. Na Mwisho amewatakia heri ya Mwaka Mpya watanzania wote
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa