Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa (MCC), Ndugu Hassan Wakasuvi kwenye mapokezi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko katika uwanja wa ndege Tabora, Novemba 18, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa (MCC), Ndugu Hassan Wakasuvi wakimpokea Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko aliyewasili katika uwanja wa ndege Tabora, Novemba 18, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akisalimiana na kumkaribisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Tabora, Novemba 18, 2023.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Tabora waliofika kwenye mapokezi uwanja wa ndege Tabora, Novemba 18, 2023.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya usalama ya Mkoa wa Tabora waliofika kwenye mapokezi uwanja wa ndege Tabora, Novemba 18, 2023.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akiangalia na kufurahia nyimbo iliokuwa ikiimbwa na Kwaya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) waliofika kumpokea kwenye uwanja wa ndege Tabora, Novemba 18, 2013.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili mkoani Tabora ambapo kesho atashiriki katika Sherehe za kumpongeza Mhasham Askofu Mkuu Mstaafu Paul R. Ruzoka na kumtakia Matashi mema Askofu Mkuu Mpya wa Tabora, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa. Sherehe zitafanyika katika Jimbo Kuu Kanisa Katoliki Tabora.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa