Chama kikuu cha Ushirika Milambo kilicho na makao makuu yake Wilayani Urambo kinatarajia kuzindua ofisi yake ya kisasa hapo kesho Machi 26, 2024.
Akiongea na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Chama Kikuu wa Ushirika Milambo Bwan. John Ntezilyo amesema ofisi hiyo ya kisasa iliyogharibu zaidi ya milioni mia 3 inatarajiwa kuzinduliwa na Mrajisi Mkuu wa Vyama vya Ushirika Dkt. Edson Ndiege na kushuhudiwa na viongozi wengine wa kiserikali ngazi ya mkoa na wilaya.
Aidha Mwenyekiti John amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo kwa kipindi cha uongozi wake, kumekuwa na mazingira mazuri katika sekta ya kilimo na kupelekea chama hiko kujenga ofisi ya kisasa ili kwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Uzinduzi wa ofisi ya chama kikuu cha Ushirika Milambo ni sehemu ya shughuli muhimu zinazotarajiwa kufanyika katika mkutano mkuu wa sita (6) wa chama hiko unaotarajiwa kufanyika kwa muda wa siku mbili (2) kuanzia kesho Machi 26, 2024.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa