• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

MSAADA WA TREKTA KUTOKA SERIKALINI KUFUNGUA MILANGO YA KITIVO CHA KILIMO NA MAZINGIRA AMUCTA – MHE. CHACHA AONGOZA HAFLA YA MAKABIDHIANO.

Posted on: June 10th, 2025

TABORA – Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuonesha dhamira yake ya kuinua elimu ya juu na sekta ya kilimo nchini baada ya kukabidhi matrekta mawili kwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mihayo cha Tabora (AMUCTA). Hafla hiyo ya makabidhiano imeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Chacha, katika viwanja vya chuo hicho, ikihudhuriwa na wanafunzi, viongozi wa chuo, pamoja na viongozi kutoka ngazi ya mkoa na wilaya.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha AMUCTA, Rev. Prof. Juvenalis Asantemungu, ametoa shukrani za dhati kwa serikali, hasa kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kufanikisha upatikanaji wa matrekta hayo. Profesa Asantemungu ameeleza kuwa msaada huo umetokana na ombi rasmi walilowasilisha kwa Waziri Bashe alipohudhuria mahafali ya kumi ya chuo hicho kama mgeni rasmi mnamo Novemba 23, 2024.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt. John Mboya, katika salamu zake za awali, alieleza kuwa changamoto ya msingi katika elimu ya juu kwa sasa ni kutokuwepo kwa mafunzo yanayokidhi mahitaji halisi ya soko la ajira. Alisema kuwa kupitia kitivo hicho kipya, AMUCTA itakuwa na mchango mkubwa katika kuandaa wahitimu watakaoweza kujiajiri kupitia ujuzi kwa vitendo, hivyo kupunguza tatizo la ajira miongoni mwa vijana.

Mkuu wa Mkoa, Mhe. Paul Chacha, alitumia fursa hiyo kuipongeza AMUCTA kwa hatua yake ya kimkakati ya kupanua maeneo ya mafunzo. Alisema hatua hiyo ni kielelezo cha weledi na uongozi thabiti wa chuo hicho. Akimwakilisha Waziri wa Kilimo, Mhe. Bashe, Mkuu wa Mkoa alisoma ujumbe maalum kutoka kwa Waziri huyo, ukisisitiza kuwa msaada huo ni mwanzo wa ushirikiano mpana kati ya wizara na taasisi hiyo ya elimu. Aliwahakikishia viongozi wa chuo kuwa serikali iko tayari kushirikiana nao katika jitihada zote za kuendeleza elimu ya kilimo, na akawahimiza kuto kusita kuwasilisha mahitaji yao kwa serikali.

Kwa niaba ya jumuiya ya AMUCTA. Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Rev.Prof. Emmanuel Wabanhu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mhe. Bashe kwa msaada huo mkubwa kwani utakwenda kuwanufaisha wanafunzi wa Imani zote kwani chuo hicho kinapokea watanzania wote bila kujali dini wala  itikadi ya mtu.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MHE, CHACHA AKEMEA UZEMBE NA KUTOWAJIBIKA KWA BAADHI YA WATUMISHI WA SHULE YA WASICHANA TABORA

    June 10, 2025
  • MSAADA WA TREKTA KUTOKA SERIKALINI KUFUNGUA MILANGO YA KITIVO CHA KILIMO NA MAZINGIRA AMUCTA – MHE. CHACHA AONGOZA HAFLA YA MAKABIDHIANO.

    June 10, 2025
  • WATUHUMIWA 11 MBARONI KWA KUJIHUSISHA NA KILIMO CHA BANGI KATIKA ENEO LA HIFADHI YA MTO IGOMBE – TABORA.

    June 09, 2025
  • TABORA YAHITIMISHA MASHINDANO YA UMISSETA: MANISPAA YA TABORA YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA KATIKA MASHINDANO HAYO NGAZI YA MKOA

    June 06, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa