Mwenge wa Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Septemba 15, 2023 umepokelewa Wilayani Tabora, ukitokea Wilayani Sikonge na kuanza kukimbizwa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kwa ajili ya kukagua,kuona, kuzindua pamoja na kuweka Mawe ya Msingi katika miradi sita (6),ya Maendeleo ikiwemo ya Elimu, Afya, Maji na Barabara yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.5
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Simon Chacha aliupokea Mwenge huo ambao ulikimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge umbali wa kilomita 60.
Mwenge wa Uhuru uliwasili Mkoani Tabora Septemba 14, 2023 na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Kiloli, Wilayani Sikonge ambapo utahitimisha mbio zake ukiwa umezindua jumla ya miradi 50 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 22.2, katika Halmashauri zote nane (8) na kukabidhiwa Mkoa wa Singida Septemba, 21, 2023.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa