Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian amekabidhi magodoro arobaini na saba (47) na mablanketi arobaini na saba (47) kwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tabora kwa ajili ya matumizi ya Gereza kuu la Uyui, ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka arobaini na saba (47) ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Februari 5, 2024.
Akikabidhi msaada huo, Mheshimiwa Batilda amesema, msaada huu wa magodoro arobaini na saba (47) ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambayo yalifanyika hapo jana Februari 4, 2024.
Akipokea magodoro hayo kwa niaba ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Gereza Kuu Uyui ACP Modest Maghande Rweyemamu amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa msaada huo na kumuahidi kwenda kuyatunza magodoro na mablanketi hayo.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa