• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC TABORA ATOA ELIMU YA FAIDA YA CHANJO KWA WAFANYABIASHARA WA MNADA WA USHIRIKA MJINI NZEGA

Posted on: October 4th, 2021

WAFANYABIASHARA katika Mnada wa Ushirika ulipo Mjini Nzega washauriwa kuchangamkia chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 ili waendelee kuwa salama na kuendesha shughuli zao za kujiingizia kipato halali.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani wakati wa ziara yake inayoendelea ya utoaji wa elimu umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 katika maeneo mbalimbali za Mkoa huo.

Alisema afya mtaji muhimu kwa kila mwanadamu na pindi anapokuwa mgonjwa shughuli zake zinateteleka na kurudisha nyuma maendeleo yake.

Balozi Dkt. Batilda Buriani alisema hivyo chanjo ya UVIKO 19 ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameileta ni salama na muhimu katika kulinda afya za wananchi na kuwawezesha kuchapa kazi bila matatizo.

Alisema Rais Samia anawapenda wananchi wake na ndio maana ameamua kuwatafutia chanjo dhidi ya ugonjwa hatari wa UVIKO 19 ambao umeshapoteza nguvu kazi na kuzorotesha uchumi wa dunia.

Balozi Dkt. Batilda alisema kuwa watu waliochanja wako katika mazingira mazuri ya kutopoteza maisha hata kama wakipata maambukizi ya UVIKO 19 , lakini wale ambao hawachanji wako kwenye uwezekano mkubwa wa kupoteza maisha pindi watakapopatwa na ugonjwa  huo.

Mkuu huyo wa Mkoa aliwaagiza watendaji katika sekta ya Afya kusogeza huduma za chanjo ya kujikinga na UVIKO 19 karibu na maeneo ambayo watu wengi wanaendesha shughuli zao za kujitafutia ridhiki.

Alisema umbali wakati mwingine umechangia baadhi ya wananchi kutoshiriki zoezi hilo la chanjo.

Baadhi ya Wafanyabiashara katika Mnada huo wameishukuru Serikali ya Mkoa wa Tabora kwa kuwapa elimu kuhusu chanjo kwa  kuwa hapo awali walikuwa hawana elimu sahihi jambo lililowafanywa kuchelewa kuchanja.

Walisema baada ya kudhibitishwa na Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora kuwa Rais Samia amechanja na viongozi mbalimbali wamechanja na chanjo ni salama wako tayari na kupata chanjo hiyo.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BARAZA LA BIASHARA MKOA WA TABORA LADHAMIRIA KULETA MAGEUZI KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KWA WANANCHI

    May 21, 2025
  • VIONGOZI WA MIKOA YA TABORA NA KIGOMA WAFANYA KIKAO CHA MAANDALIZI KUELEKEA MAONESHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA NANE NANE 2025

    May 20, 2025
  • RC CHACHA AZINDUA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA MKOA WA TABORA, ATOA WITO WA KULINDA NDOTO ZA WATOTO.

    May 19, 2025
  • TABORA YAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA FAMILIA KWA KUTOA WITO WA MALEZI BORA NA KUPINGA UKATILI.

    May 15, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa