• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC TABORA AWATAKA WATAALAMU KUSAIDIA WALENGWA WA TASAF KUTUMIA FEDHA ZAO KUIBUA MIRADI

Posted on: July 8th, 2021

RC TABORA AWATAKA WATAALAMU KUSAIDIA WALENGWA WA TASAF KUTUMIA FEDHA ZAO KUIBUA MIRADI

MKUU  wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewaagiza Wataalamu kusaidia katika utoaji wa elimu ya matumizi sahihi ya fedha wanazopatiwa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini(TASAF) ili waweze kuanzisha miradi itakatowaendeleza wenyewe.

Aliota kauli hiyo jana wakati wa Kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF na kutoa mwongozo wa utambuzi na uandikishaji wa kaya za walengwa katika eneo la Utekelezaji kwenye Manispaa ya Tabora.

Alisema fedha wanazopata walengwa wanaweza kuzitumia katika shughuli mbalimbali ikiwemo ufugaji wa nyuki, kuku na mifugo mingine ambayo itawakomoa na kuwafanya wapande daraja na kuacha kutegemea ruzuku ya Serikali.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kupitia TASAF kaya zaidi milioni 1 zimenufaika na kufanyakazi za ujasiriamali na kuweza kuendesha maisha yao kwa unafuu ukilinganisha na awali.

Balozi Dkt. Batilda alisema Mkoa wa Tabora unazofursa nyingi kama vile mistu mikubwa , ardhi ya kutoa na mifugo mingi ambapo walengwa wanaweza nao kutumia nafasi hizo kusonga mbele kimaisha.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa aliagiza kufungwa kwa Kamera za ulinzi(CCTV  Camera ) katika maeneo makubwa ya biashara ikiwemo minadani masokoni ili kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali.

Alisema sanjari na hilo ni vema Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ikaimarishwa ili kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Balozi Dkt. Batilda alisema alisema katika maeneo ambayo yamefungwa mifumo ya TEHAMA imeonyesha mafanikio makubwa ambapo mapato ya Serikali yapanda mara tatu ya awali.

Awali Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) Gerald Macha alisema utambuzi wa awamu utafanywa kwa makini na wahusika watakula kiapo ili kuepuka kuingiza majina ya watu wasiostahi

MWISHO

Matangazo

  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • TANGAZO LA KAZI ZA MUDA ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI WA SENSA 2022 May 06, 2022
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • NAMBA ZA MAWASILIANO OFISI YA MKOA TABORA November 23, 2020
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MKUU WA MKOA WA TABORA MH. BALOZI DKT BATILDA S. BURIANI AFUNGUA KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE NGAZI YA MKOA

    July 22, 2022
  • WATU WAPOTEZA MAISHA WILAYANI SIKONGE BAADA YA KUFUNIKWA NA KIFUSI

    November 19, 2021
  • RC TABORA ASEMA WAKAZI WA URAMBO KUPATA MAJI KWA ASILIMI 95 IFIKAPO MWAKA 2025

    November 08, 2021
  • RC TABORA AAGIZA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUTOA ELIMU YA UJASIRIAMALI KWA WALENGWA WA TASAF

    November 03, 2021
  • Angalia zote

Video

JPM BANDARINI
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • Government Portal
  • SALARYSLIP

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa