RC TABORA: TUDIZI KUMUOMBEA MH.RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN.
_________________________
Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Balozi Dkt. Balozi Batilda Salha Burian amewataka waumini wa dini mbalimbali kuzidi kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan ili aweze kutekeleza mipango ya maendeleo ya taifa letu.
Ameyasema hayo wakati alipohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na kampuni ya Mkwawa Tobacco Leaf kwa kushirikiana na Baraza La Waislamu Tanzania ( BAKWATA) mkoa wa Tabora. Amewataka viongozi wa dini mbalimbali kusimamia masuala ya maadili hasa kwenye kipindi hiki ambacho taifa linakabiriliwa na mmomonyoko wa maadili.
Aidha ameipongeza kampuni ya Mkwawa Tobacco Leaf kwa kushirikiana na BAKWATA mkoa wa Tabora kwa kutembelea na kutoa misaada (sadaka) kwa baadhi ya vituo vya watoto wenye mahitaji maalumu.
Hii ni mara ya pili Dkt. Batilda Burian kuhudhuria hafla ya futari, ambapo hafla ya kwanza alihudhuria tarehe 05/04/2023 iliyoandaliwa na Benk ya CRDB.
_______________________
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa