• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

Wilaya ya Urambo

Wilaya ya Urambo

  

        

      

                                    

UTANGULIZI

  • Wilaya ya Urambo ni kati ya Wilaya 7 zinazounda Mkoa wa Tabora. Wilaya hii ilianzishwa tarehe 19/07/1975, ina tarafa 2 ( Ussoke na Urambo ) ina ukubwa wa eneo lenye km2 6,110 sawa na 8% ya eneo la Mkoa, Makao makuu ya Wilaya yapo katika mji mdogo wa Urambo umbali wa km 90 kutoka Tabora Mjini.

  •  Wilaya hii imepakana na Wilaya ya Sikonge na Uyui kwa upande wa Mashariki, na inapakana na Wilaya ya Mpanda (Mkoa wa Katavi) kwa upande wa Kusini, kwa upande wa Kaskazini Magharibi inapakana na Wilaya ya Kaliua.

IDADI YA WATU. 

  • Kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Wilaya ya Urambo ina jumla ya wakazi wapato 192,781. Kati yao Wanaume 95,997 sawa na 49.80% na Wanawake 96,784 sawa na 50.2% . Wilaya ina jumla ya kaya 32,675 kwa wastani wa ukubwa wa kaya moja ni watu 5.9 ongezeko la watu kwa mwaka inakisiwa kuwa 4.8%. 

HALI YA UCHUMI NA MAENDELEO YA WILAYA. 

  • Uchumi wa Wilaya unategemea zaidi kilimo ambacho kinaajiri takribani asilimia 80 ya wakazi wote wa Wilaya hii. Mapato yanayotokana na ufugaji, Uvuvi, Ufugaji wa nyuki na shughuli za viwanda vidogo vidogo ni ajira mbadala zinazochangia katika pato la wakazi wetu. 

  • Pato la Wilaya ya Urambo katika mwaka 2012/2013 hadi Desemba, 2012 lilikuwa Tshs. 77,822,778,064/= ikilinganishwa na idadi ya watu 192,781 na hivyo pato la mtu ni sawa na Tshs. 403,685/=. Aidha wastani wa pato la mtu kwa mwaka liliongezeka kutoka Tshs. 172,000/= mwaka 2002 hadi Tshs. 403,685/= mwaka 2012, sawa na ongezeko la Tshs. 231,685/=. 

HALI YA ULINZI NA USALAMA 

  • Hali ya ulinzi na usalama katika Wilaya yetu kwa ujumla ni nzuri; na hii inachangiwa na uwepo wa ulinzi shirikishi kupitia Polisi jamii. Mpango huu muhimu ni wa kudumu kwa kushirikisha jeshi la mgambo katika suala la ulinzi kwa kuwatambua, kuwajali na kuwathamini.

  • Hata hivyo wilaya inaendelea kukabiliana na matukio mara kwa mara ya makosa ya jinai yakiwemo ya unyang’anyi wa kutumia silaha na nguvu, Uvunjaji, Wizi wa pikipiki,Wizi wa mifugo,kuchoma nyumba moto n.k. Mauaji yanayotokea katika Wilaya hii mara nyingi yanatokana na kulipiza kisasi, imani za kishirikina na matukio machache ya kugombea mali.

  • Kufuatia hali hiyo wilaya inashirikiana na Wilaya jirani katika mkakati wa kuimarisha Ulinzi na usalama na kubadilishana taarifa za kiuharifu miongoni mwetu na Wilaya zinazotuzunguka. 

HALI YA UTOAJI HUDUMA KISEKTA

  • Shughuli ambazo zimekuwa zikitekelezwa na Wilaya kisekta katika utoaji wa huduma za kijamii na kiuchumi kama ifuatavyo:-

SEKTA YA UTAWALA NA UTUMISHI. 

  • Wilaya ina jumla ya watumishi 1,458 kutoka katika kada mbalimbali za utumishi kama zifuatavyo:- Utawala na Utumishi 100, Elimu Sekondari 209,Elimu Msingi 835 , Afya 215, Kilimo Umwagiliaji na Ushirika 15,Mifugo na Uvuvi 9,Ardhi na Maliasili 6, Maji 7, Ujenzi 18, Watendaji wa Vijiji 43 na Usafi na Mazingira 1.

  • CHANGAMOTO

  1. Watumishi walioajiriwa kuomba kuhama kufuata wenzi wao baada ya kukaa muda 

  2. Ufinyu wa bajeti 

  3. Utoro kazini 

  4. Watumishi wapya Kushindwa kuripoti na Serikali kutoleta watumishi kulingana na ikama iliyoidhinishwa.




Matangazo

  • WALIOCHANGULIWA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA TABORA December 14, 2022
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • NAMBA ZA MAWASILIANO OFISI YA MKOA TABORA November 23, 2020
  • Angalia zote

Habari mpya

  • CCM TABORA WARIDHISHWA NA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM YA MWAKA 2020-2025

    March 20, 2023
  • UFUNGUZI WA KIKAO CHA TATHMINI YA MAENDELEO YA MKOA(RCC)

    February 21, 2023
  • UTIAJI SAINI MKATABA WA UJENZI WA MABWAWA YA KUTIBU MAJITAKA

    February 22, 2023
  • KALIUA TABORA

    January 05, 2023
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • Government Portal
  • SALARYSLIP

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa