Akitoa hotuba yake, Mkuu wa Mkoa wa Tabora ametoa maelekezo kwa Wakurugenzi wote Mkoani Tabora kwa kuwatumia Maafisa Ustawi wa Jamii kuhakikisha wanawatambua watu wenye ulemavu ili kutoa nafasi kwa Serikali na wadau wake kuwahudumia na kutimiza mahitaji yao
“Wakurugenzi wawaelekeze Maafisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri zote za Mkoa wa Tabora, kuendelea kuwatambua na kubaini mahitaji ya watu wenye ulemavu na kuwatimizia mahitaji yao” alielekeza Mhe. Mkuu wa Mkoa
Sambamba na hilo Dkt. Batilda ameendelea kutoa maelekezo kwa wakurugenzi kutenga fedha kwa ajili ya vikao kazi ili kuwawezesha watu wenye ulemavu na taasisi mbalimbali zinazohudumia watu wenye ulemavu.
“Naendelea kutoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri watenge fedha kwa ajili ya kuwezesha kufanyika kwa vikao vya kisheria vya kamati za kuhudumia watu wenye ulemavu kwa ngazi za Halmshauri na Kata. Vikao hivi vitasaidia sana kubaini mahitaji ya watu wenye ulemavu” alieleza Dkt. Batilda.
Aidha Mhe. Mkuu wa Mkoa amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya watu wenye ulemavu na viongozi wa Mkoa watahakikisha wanasimamia fedha hizo kikamilifu
“Napenda kutoa shukrani zangu kwa Mhe. Rais wetu kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya watu wenye ulemavu” alisema Mhe. Mkuu wa Mkoa.
Ikumbukwe kuwa Mweyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi JTI Anna Makinda alimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian vifaa vya watu wenye ulemavu vikiwemo magongo ya kiwiko jozi 50, magongo ya makwapani jozi 48, baskeli za maguludumu (miguu) matatu 2 na mguu wa bandia Mmoja (1) vyenye thamani ya Shilingi Milioni 11.1.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akimkabidhi mmoja ya Watu wenye Ulemavu Baskeli yenye maguludumu matatu maalumu kwa Watu wenye Ulemavu katika Hafla ya kukabidhi Vifaa Saidizi kwa watu wenye ulemavu iliyofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi Disemba 6, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akimkabidhi mmoja ya Watu wenye Ulemavu fimbo maalumu ya kutembelea kwa Watu wenye Ulemavu katika Hafla ya kukabidhi Vifaa Saidizi kwa watu wenye ulemavu iliyofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi Disemba 6, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akimkabidhi mmoja ya Watu wenye Ulemavu magongo ya makwapani maalumu kwa kutembelea kwa Watu wenye Ulemavu katika Hafla ya kukabidhi Vifaa Saidizi kwa watu wenye ulemavu iliyofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi Disemba 6, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Salha Burian akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi wa Watu wenye Mahitaji Ulemavu mara baada ya Hafla ya kukabidhi Vifaa Saidizi kwa watu wenye ulemavu iliyofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi, kumalizika Disemba 6, 2023.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa