• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

Miombo








0. UTANGULIZI

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Misitu ya Miombo (SFM) unatekelezwa kwa muda wa miaka mitano kuanzia mwaka 2013 hadi 2018.Ufadhili wa Mradi huu ni kutoka Mfuko wa Mazingira Duniani kwa kukasimu usimamizi wa fedha katika Shirika la Maendeleo la Dunia (UNDP) ofisi ya Tanzania iliyopo Dar es Salaam. Kwa upande mwingine Mradi umefadhiliwa na serikali ya Tanzania kwa kukasimu majukumu katika ofisi ya Makamu wa Rais ambapo utekelezaji wa shughuli unasimamiwa na ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Tabora akishirikiana na Katibu Tawala Mkoa wa Katavi.Utekelezaji wa shughuli katika ngazi ya jamii unafanywa na Halmashauri za Wilaya ya Kaliua,Urambo na Uyui kwa Mkoa wa Tabora na Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kwa Mkoa wa Katavi. Aidha Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Tathmini ya Rasilimali za Maliasili (IRA) pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii Idara ya Misitu na Nyuki ilipewa jukumu la uangalizi na ushauri wa kitaalam katika utekelezaji.

  • JINA LA MRADI 
  •  
  • Usimamizi Endelevu wa Misitu ya Miombo katika Ukanda wa magharibi mwa Tanzania, Mkoa wa Tabora na Katavi.
  • LENGO KUU
  •  
  • Kuwa na usimamizi endelevu wa misitu itakayofanya bayoanui na ikolojia kuwepo, misitu kinga ya misitu iliyoko Kongo iletayo mvua, kuwa na uhakika wa chakula na maisha bora kwa jamii.
  • LENGO MAHSUSI LA MRADI
  • Kuwezesha jamii inayotegemea misitu ya miombo kuwa na njia bora za uzalishaji ambazo zitasababisha hifadhi ya bayoanuai, kupungua kwa uzalishaji wa hewa ukaa kutokana na matumizi ya ardhi na hatimaye kuboresha hali ya maisha kwa jamii.
  • ENEO LA UTEKELEZAJI WA MRADI 
  •  
  • Mradi ulipanga kusimamia eneo linalokadiliwa kuwa na hekta 133,400 toka katika Vijiji 28 vyenye kaya 15,530, Kata 4 za Usinge, Imalamakoye, Mbola Cluster (kata 6) zilizoko katika wilaya za  Urambo na Uyui katika Mkoa wa Tabora na kata ya Inyonga katika wilaya ya  Mpanda katika Mkoa Katavi. Mradi umetekelezwa na kusimamia eneo lenye ukubwa wa hekta  290,788.3 kwa njia ya usimamizi shirikishi (CBFM/JFM) toka katika vijiji 42 vyenye kaya 16,096 Kata 13 toka katika Wilaya 4 za Kaliua, Urambo, Uyui na Mlele zilizoko katika Mikoa ya Tabora na Katavi. Mabadiliko ya kiutawala yaliongeza idadi ya wilaya, Kata na Vijiji katika eneo linalotekelezwa na Mradi.
  • RAMANI YA ENEO LA MRADI


  • NYANJA ZA UTEKELEZAJI WA MRADI 
  • Kuboresha Sera za Taifa zinazorandana na Usimamizi Endelevu wa Misitu kama vile Sera ya Misitu, Sera ya Kilimo, Sera ya Mifugo na Sera ya Wanyamapori.
  • Kujenga uwezo katika Usimamizi Shirikishi wa Misitu, Kilimo bora na Matumizi bora ya ardhi.
  • Kuwezesha jamii kuzalisha mkaa mbadala vilevile kuwa na matumizi sahihi ya nishati katika usimamizi endelevu wa misitu.
  • Uboreshaji wa uchumi  wa jamii kwa kuimarisha masoko na mnyororo wa thamani wa mazao yasiyotimbao kama nta,asali,uyoga na mazao ya kilimo kama vile alizeti, karanga na mahindi.Pia kuweka mfumo wa upatikanaji wa mitaji kwa jamii kupitia VICOBA na pia  Ushirika kwa ajili ya kujenga uwezo kupata pembejeo kwa bei nafuu na kuuza mazao kwa bei nzuri.
  • MAFANIKIO NA MIFANO YA KIUGWA 
  • Mradi umewezesha utungaji na matumizi ya sheria ndogo katika usimamizi endelevu wa misitu na matumizi bora ya ardhi. Vijiji 19 kati ya Vijiji 22 tarajiwa vimetunga sheria na vinatumia katika usimamizi wa misitu ya Vijiji. Kwa upande wa matumizi bora ya ardhi Vijiji 9 kati ya 10 vilivyolengwa vina sheria ndogo za usimamizi.
  • Mradi umewezesha uanzishaji na kupandisha hadhi eneo lenye ukubwa wa hekta 5085 kuwa na misitu 8 ya Vijiji na msitu 1 wa Gereza la Kilimo la Nsenda lililopo Wilaya ya Urambo. Eneo la msitu wa North Ugalla katika Vijiji vya Mtakuja, Utenge na Kangeme vilivyopo katika wilaya ya Urambo, limeidhinishwa kuwa na usimamizi wa pamoja (JFM) kati ya vijiji tajwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS). Misitu ya Vijiji inasimamiwa na jamii (CBFM) na Msitu wa Gereza unasimamiwa na Taasisi ya Gereza wakiwa ni wamiliki na wanufaika wa misitu kwa asilimia mia moja, ambapo msitu wa Ugalla unamilikiwa na TFS na Wanufaika ni Vijiji husika na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa mgao uliopo katika makubaliano ya pamoja (JMA).
  • Uanzishaji wa kamati za maliasili katika vijiji 42 zenye jumla ya wajumbe 504 na kamati za matumizi bora ya ardhi katika vijiji 9 zenye jumla ya wajumbe 63 ambao wapo katika muundo wa serikali za  Vijiji kwa mujibu wa Sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982.
  • Uwezeshaji wa shughuli za kuongeza kipato kwa jamii kama vile:-
  • Ufugaji wa nyuki katika vikundi 31 vilivyopo katika wilaya za Kaliua,Urambo,Uyui na Mlele na mshine 1 ya kisasa ya uchakataji asali iliyopo Inyonga – Mlele.Uzalishaji wa mazao ya nyuki kama asali imeongezeka kutoka kilo 118,120 (mwaka 2014) hadi kilo  122,017.5 (mwaka 2017) sawa na Tsh. 976,568,000. Nta imeongezeka kutoka kilo 7,805 (mwaka 2015) hadi kilo 8,337 (mwaka 2017).
  • Usindikaji/uchakataji wa matunda pori (Jam, Juisi, madawa ya asili nk.) umeongezeka kutoka wastani wa kilo 625 (mwaka 2013) Mradi unapoanza hadi kufika kilo 976 (mwaka 2017) kwa mwaka katika kikundi cha MEMBO kilichopo kijiji cha Mbola wilaya ya Uyui Mkoa wa  Tabora.
  • Kilimo bora cha alizeti katika wilaya ya Kaliua,Urambo,Uyui na Mlele na uwezeshwaji wa mashine 1 ya usindikaji wa alizeti katika kijiji cha Kombe wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora na mashine 1 katika kijiji cha  Inyonga wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi.
  • Kilimo cha mahindi uzalishaji wa awali ulikuwa tani 1.3 (mwaka 2014) kwa ekari 1 na kuongezeka hadi  tani 1.8 kwa ekari (mwaka 2017) katika katika wilaya za Kaliua,Urambo,Uyui na Mlele.
  • Ufugaji wa samaki katika mabwawa 3; bwawa 1 kwa kila wilaya za Urambo (mwaka 2017) na Kaliua (mwaka 2018) katika Mkoa wa Tabora na wilaya ya Mlele (mwaka 2018) katika Mkoa wa Katavi kwa kupanda jumla ya vifaranga vya samaki 7,000.
  • Uzalishaji wa mkaa mbadala katika wilaya za Urambo, Kaliua,Uyui na Mlele) kwa kutumia mashine ndogo za umeme na mikono zikizalisha jumla ya kilo 9660 za mkaa mbadala (briquettes) kwa mwaka 2017. Na pia mashine kubwa ya kisasa ya kutengeneza mkaa mbadala (briquettes) iliyosimikwa  katika kijiji cha Ilolanguru wilaya ya Uyui yenye uwezo wa kuzalisha wastani wa kilo 350 kwa saa (mwaka 2018).
  • Mradi umeanzisha jumla ya VICOBA 17 kwa ajili ya upatikanaji wa mitaji kwa jamii vyenye akiba ya kuanzia Tsh. 4,170,000   hadi Tsh. 21,000,000 ambapo kuna wajumbe 379 (wanaume109 na wanawake 270). Baada ya kukamilisha mzunguko wa fedha wa mwaka 2017, VICOBA 10 vimewezeshwa mtaji wa Tsh.616,000 kwa kila kimoja katika mwaka 2018.
  • Mradi umeunda Vyama vya Ushirika 6 vyenye wanachama 321 (wanawake 120 na wanaume 201) visivyojishughulisha na kilimo cha zao la Tumbaku na badala yake ni mazao ya alizeti, mahindi na karanga kwa ajili ya kujenga uwezo kupata pembejeo kwa bei nafuu, kufuata kanuni bora za kilimo na kupata masoko ya uhakika kwa urahisi.
  • Mradi umewezesha ufugaji wa kuku kwa  uzalishaji wa kuku chotara kwa ajili ya nyama na mayai. Wafugaji 14 wamewezeshwa ujenzi wa mabanda ya kuku na kupatiwa jumla ya kuku 1,445 (jogoo 1,025 na tetea 420) pia  chanjo na madawa katika wilaya za Urambo, Kaliua, Mlele na Uyui.
  • Uendelezaji wa teknolojia ya utengenezaji wa sabuni kwa vikundi 2 katika wilaya ya Urambo.Aidha wastani wa uzalishaji  kwa mwanakikundi ni miche 7200 ikiwa kila mche ni Tsh.1000 ni sawa na Tsh.7,200,000 kwa mwaka.
  • MATARAJIO BAADA YA MUDA WA MRADI KUISHA
  •  
  • Utekelezaji wa Mradi utaendelea kusimamiwa na halmashauri nne za wilaya za Kaliua, Urambo na Uyui katika Mkoa wa Tabora na Mlele katika Mkoa wa Katavi.
  • Kamati za Maliasili za vijiji (VNRCs) na za Matumizi bora ya ardhi ya vijiji (VLUM) zilizoundwa zitaendeleza utekelezaji wa shughuli husika kwani ni kamati za kudumu katika muundo wa serikali za vijiji kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982.
  • Ufuatiliaji na ushauri utaendelea kusimamiwa na ngazi ya Mkoa (RTTs) wa Tabora na Katavi.
  • Mafanikio ya shughuli zilizotekelezwa na Mradi yataendelezwa na wadau mbalimbali kama vile Taasisi za kiserikali (TFS, Chuo cha Nyuki-Tabora, SIDO,TASAF na Chuo cha Utafiti wa Kilimo Tumbi) na Taasisi zisizo za kiserikali (ECO Village, Makampuni ya Tumbaku kama vile TLTC,JTI, Alliance One, Premium,).
  • Kutakuwa na Mradi mwingine “Scaling up livelihood activities into the naturalized Tanzanians living in Miombo Woodlands of Western Tanzania”  utakaotekelezwa katika maeneo ya makazi ya wakimbizi ya Ulyankulu katika Mkoa wa Tabora na Katumba na Mshamo katika Mkoa wa Katavi.
  • Matumizi ya nyaraka muhimu za Mradi (kama vile andiko la Mradi, makala  ya Mradi, utafiti wa udongo kwa mazao mbalimbali, sheria ndogo za usimamizi wa misitu na matumizi bora ya ardhi,tathmini shirikishi za raslimali za misitu, mipango ya usimamizi wa misitu na vitini vya mafunzo katika nyanja za Mradi).

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BODI YA WADHAMINI MFUKO WA MISITU TANZANIA YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO TABORA.

    May 07, 2025
  • NAIBU WAZIRI MKUU AONGOZA HAFLA YA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KIWANDA CHA NGUZO ZA ZEGE TABORA.

    May 03, 2025
  • DKT. BITEKO AIPONGEZA TANESCO NA ETDCO KWA JUHUDI ZA KUBORESHA HUDUMA YA UMEME URAMBO

    May 02, 2025
  • SERIKALI IPO KAZINI KUBORESHA HAKI NA MASLAHI YA WAFANYAKAZI, WAFANYAKAZI NI UTI WA MGONGO WA TAIFA – MHE. SAUDA MTONDOO,

    May 01, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa