Baba Askofu Mkuu, Muadhama Kardinali Protase Rugambwa, amefanya ziara maalum katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa lengo la kumtembelea Katibu Tawala wa Mkoa huo, Dkt. John Mboya, na kufanya mazungumzo mafupi kuhusu masuala ya maendeleo ya mkoa.
Akipokea ugeni huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Mboya alimshukuru Kardinali Rugambwa kwa heshima ya kuitembelea ofisi hiyo na kusisitiza kuwa Serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana na Kanisa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na taasisi hiyo kwa ustawi wa wananchi.
Kwa upande wake, Kardinali Rugambwa alieleza dhamira ya Kanisa kuendeleza ushirikiano na Serikali katika kutoa huduma na kutekeleza miradi ya maendeleo. Aidha, alisisitiza kuwa Kanisa litaendelea kuhamasisha na kualika wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza mkoani Tabora ili kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Ziara hiyo ya Muadhama Kardinali Rugambwa imeonesha mshikamano na upendo wa dhati kati ya Serikali na taasisi za kidini katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hatua inayotarajiwa kuongeza ari ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi wa Mkoa wa Tabora.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa