• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
      • Community development
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC CHACHA AFUNGUA KONGAMANO LA WAFANYABIASHARA WADOGO MKOA WA TABORA, AWASIHI WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA ZA ZABUNI ZA SERIKALI

Posted on: September 24th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Matiko Chacha, ameongoza na kufungua rasmi kongamano la wafanyabiashara wadogo mkoani humo lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Utumishi wa Umma – Uhazili, ambapo amewataka wananchi wa Tabora kuchangamkia kwa ujasiri fursa za kiuchumi zinazotolewa na Serikali kupitia mfumo wa manunuzi ya umma (NeST) pamoja na kuchangamkia mitaji kupitia mikopo isiyo na riba inayotolewa na serikali.


Akitoa neno la utangulizi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dkt. John Mboya, alimshukuru Mhe. Chacha kwa kukubali kuwa mgeni rasmi, akisisitiza kuwa kongamano hilo lina umuhimu mkubwa kwa ustawi wa kiuchumi wa wananchi, hususan wafanyabiashara wadogo. “Jukwaa hili ni mahsusi kwa ajili ya kuwawezesha ninyi wananchi kutambua fursa nyingi ambazo serikali yetu imeziweka kupitia sera na sheria mbalimbali, hivyo ni muhimu kusikiliza kwa makini ili tuweze kunufaika nazo,” alisisitiza Dkt. Mboya.


Akitoa salamu kutoka Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA) makao makuu, Meneja wa PPRA Kanda ya Magharibi na Kati, Mhandisi Suma Atupele, alieleza kuwa kifungu cha 64 cha Sheria ya Ununuzi wa Umma na Kanuni ya 35 kinatoa mwongozo wa namna zabuni za serikali zinavyopaswa kutekelezwa kwa makundi maalum, yakiwemo wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu. Alibainisha kuwa ni wajibu wa kila taasisi za serikali kutenga angalau asilimia 30 ya zabuni kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo, hivyo akatoa wito kwa wananchi kujisajili ili kunufaika na fursa hiyo adhimu.


Mratibu wa Mfuko wa Programu za Uwezeshaji kutoka NEEC, Ndg. Samwel Shikona, alisema serikali imeweka miongozo na sheria thabiti za kuwawezesha wananchi kiuchumi. Alibainisha jukumu lao kubwa ni kuwaunganisha wananchi na fursa zilizopo nchi nzima ili washiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.


Akihutubia washiriki wa kongamano hilo, Mhe. Chacha aliwasisitiza wananchi kujenga kujiamini na kuchukua hatua madhubuti katika kuchangamkia fursa hizo. “Kwanza tujiamini na kuwa serious. Wataalamu wapo kutusaidia, tuhakikishe tunajisajili ili hizo fursa za asilimia 30 zisitupite. Hali ya usalama wa mkoa wa Tabora ipo shwari, tuchangamkie fursa, tufanye biashara na kujipatia kipato. Hakuna hela ya muujiza; wewe fanya kazi. Mganga wa kienyeji hawezi kukuletea pesa, hebu fanyeni yale ambayo serikali inawaambieni,” alisisitiza Mhe. Chacha.


Kongamano hilo limejikita katika kuhamasisha wananchi, hasa wafanyabiashara wadogo wa Tabora, kushiriki kikamilifu kwenye fursa za kiuchumi na kimaendeleo zinazotolewa na serikali kupitia sera na mifumo rasmi ya manunuzi na uwezeshaji.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZASOGEZWA KWA WANANCHI: MADAKTARI WABOBEZI 56 WAWASILI TABORA KUHUDUMIA WANANCHI

    September 29, 2025
  • MKOA WA TABORA WAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA ULINZI WA HAKI ZA MTOTO

    September 26, 2025
  • RC CHACHA AFUNGUA KONGAMANO LA WAFANYABIASHARA WADOGO MKOA WA TABORA, AWASIHI WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA ZA ZABUNI ZA SERIKALI

    September 24, 2025
  • MKOA WA TABORA WAPATA ALAMA YA KIJANI KATIKA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA LISHE.

    August 27, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice
  • Migration Tanzania

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa