Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Chacha, Mkuu wa Wilaya yaKaliua, Mhe. Dkt. Gerald Mongella ameongoza hafla fupi ya kuwapokea madaktaribingwa wa Mama Samia waliowasili mkoani humo kwa ajili ya kutoa huduma zakibingwa kwa wananchi katika halmashauri zote nane za mkoa. Hafla hiyoimefanyika katika ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora nakuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mganga Mkuu waMkoa wa Tabora, Dkt. Honoratha Rutatinisibwa ameishukuru Serikali ya Awamu yaSita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. SamiaSuluhu Hassan, kwa kuanzisha mpango huu wa kambi za madaktari bingwa.Amebainisha kuwa zaidi ya watumishi wa afya 367 wamepata mafunzo kazini kupitiakambi hizi na wananchi wamenufaika kwa kupata huduma karibu, hivyo kupunguzagharama kubwa za matibabu.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Wizara ya Afya,Dkt. Felix Bundala, amesema lengo kuu la kambi za madaktari bingwa nikuwasogezea huduma wananchi wa kipato cha chini, huku wakitoa mafunzo elekezikwa wataalamu wa afya katika maeneo wanayofikia. Aidha, ameongeza kuwa mpangohuu pia unasaidia kuimarisha miundombinu ya afya na matumizi ya vifaa tiba vyakisasa kwa ufanisi zaidi.
Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora,Ndg. Amos Ackim, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelezauwekezaji mkubwa katika sekta ya afya mkoani humo. Ameeleza kuwa kwa mwaka wafedha 2024/25 pekee, Tabora imepokea dawa na vifaa tiba vyenye thamani yashilingi bilioni 11, wataalamu wa afya 504 pamoja na magari 24 ya kubebeawagonjwa. Ameongeza kuwa ujio wa madaktari bingwa ni uthibitisho wa dhamira yadhati ya serikali kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Akifunga hafla hiyo, Dkt. Mongella ameishukuruserikali kwa maono na hekima ya kuanzisha mpango huu wa madaktari bingwa waMama Samia. Amesema kuanza kwa huduma hizo kumeleta msaada mkubwa kwa wananchiwa Tabora, kumeimarisha mafunzo kwa wataalamu wa afya na kuongeza ufanisikatika matumizi ya vifaa tiba. Katika awamu hii ya nne, jumla ya madaktaribingwa 56 wamewasili mkoani humo, ambapo tangu kuanza kwa mpango huu zaidi yawananchi 230,000 wamefikiwa na huduma za kibingwa katika Mkoa wa Tabora.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa