MKUU wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri ameakea vitendo vya baadhi ya Watendaji na wananchi kujichukulia Sheria mkononi kwa kupiga na kuwatesa watuhumiwa kinyume na taratibu za Sheria.
Alisema watuhumiwa wanapokamatwa na kuanza kuadhibiwa havikubaliki na Serikali itamchukulia hatua mtu atakayebainika kuchochea uvunjifu wa Sheria za kushughulikia mharifu.
Magiri alitoa kauli hiyo wakati akijibu hoja za baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge waliodai kuwa Watumishi wa Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania(TFS) wamekuwa wakikamata wananchi na kuwatesa na kuwadhalisha wanapokuwa doria.
Alisema hakuna chombo chochote isopokuwa Mahakama pekee ndio inaruhusiwa kutoa adhabu kwa watuhumiwa na kuongeza kuwa kama kuna Mfanyakazi yoyote wa TFS ambaye anatuhumiwa kumkamata mtu kwenye Hifadhi wakati wa doria na kumtesa apewe taarifa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
Magiri alisema kimisngi kuingia katika Hifadhi ya Mistu na kuvuna miti bila kibali ni makosa lakini hayahalalishi mtuhumiwa kuteswa na kudhalilishwa bali anapaswa kumpeleka Polisi na hatimaye aende Mahakaani.
Aliongeza kuwa hata wale wanaoingia katika Hifadhi ya Wanyamapori na kuua wanyama bila kibali ni wakosaji na wahusika wanatakiwa kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Sikonge aliwataka Madiwani kutoa elimu katika maeneo yao kwa wananchi wao ya kuwa kuingia katika Hifadhi za aina yoyote bila kibali ni kosa.
Alisema haipendezi wananchi wanaingia katika Hifadhi za wanayapori na mistu bila vibali na wanapokamatwa ndipo baadhi ya Madiwani na viongozi wanajitokeza kuwatetea wakati wanajua kuwa wahusika wamevunja Sheria.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Sikonge aliongeza kuwa ni vema Watuhumiwa wakimatwa wakatii Sheria maana mara nyingine kupigwa kwao kunatokana na wengine kuleta ubishi.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa