JAFO AAGIZA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUTENGA MAENEO YA UJENZI WA VIWANJA VYA MICHEZO VYA KISASA
OFISI ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) imewaagiza Wakuu wa Mikoa , Makatibu wa Mikoa, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote kuhakikisha wanabainisha maeneo makubwa ambayo yanaweza kujengwa viwanja wa michezo vyenye hadhi ya kimataifa.
Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Selemani Jafo katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Copa Cola cola UMISETA mkoani Tabora.
Alisema hatua hiyo inalenga kukuza michezo mbalimbali hapa nchini na kuongeza ajira kwa vijana.
Jafo alisema sanjari na utengaji wa maeneo ya ujenzi wa viwanja aliaagiza maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya michezo na burudani wahakikishe yasibadishwe matumizi na kuvamiwa.
Aidha Waziri huyo aliwaagiza Wakuu wa Mikoa , Makatibu wa Mikoa, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri kuhakikisha vipindi vya masomo ya michezo na masomo mengine ya burudani shukeni yafundishwa kwa nadharia na vitendo ili kuwajenga wanafunzi kuwa katika ari ya kukabiliana vema katika ushindani.
Aliongeza kuwa wanapaswa pia kuhakikisha kuwa kila Shule ina viwanja vya michezo vyenye vipimo sahihi vinavyotakiwa na kusimamia Sheria ya Elimu inayotaka Shule inaposajiliwa lazima iwe na eneo la viwanja vya michezo.
Jafo pia aliagiza kuwa Shule zilizoteuliwa kuwa na mchepuo wa michezo ziimarishwe na walimu wake wasihamishwe.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo amewataka viongozi mbalimbali wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanatekeleza agizo la Mheshimiwa Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan la kuhimiza mchakamchaka kwa wanafunzi na wananchi kufanya mazoezi kuepuka magonjwa yasiyoambukiza.
MWISHO
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa