RC ATAKA WANANCHI WASHIRIKISHWE KWENYE UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
MKUU wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati ametoa wito kwa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega na maeneo mengine kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuongeza tija.
Alisema hatua hiyo itasaidia kuilinda dhidi ya uhujuma yoyote kwa sababu wao watakuwa sehemu ya waliofanikisha kukamilika kwa mradi kutokana michango ambayo watakuwa wametoa.
Dkt. Sengati alitoa kauli hiyo katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega wakati wa ukaguzi wa miradi mitatu ambayo ni ujenzi wa Bweni la wasichana katika Sekondari ya Mwanahala, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwenye shule ya Msingi Uhemeli na ujenzi wa vyumba viwili katika Sekondari ya Kampala.
Alisema wananchi wakielimishwa na kuhamasisha kushiriki katia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao watawezesha kutekelezwa kwa miradi mingi kwa fedha ambayo inaletwa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kiwango kizuri.
Awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwanahala Agatha Mwaliwale alisema kuwa walipokea kiasi cha shilingi milioni 80 toka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana 80 ikiwa ni mkakati wa kuanzisha cha tano na Sita katika shule hiyo.
Alisema ujenzi umefikia asilimia 95 na wamekwisha tumia kaisi cha shilingi milioni 79.5 na kubakiza shilingi milioni 420.
Agatha alisema kutoka na fedha iliyobaki haiwezi kukamilisha ujenzi , Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imetenga kiasi cha shilingi milioni 20 katika bajeti ijayo kwa ajili ya shughuli zilizobaki.
Kwa upande wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Kampala , Emmanuel Majebele alisema walipokea kiasi cha shilingi milioni 46.6 ambazo zimekabilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu matano ya vyoo.
Alisema kukamilika kwa mradi huo kumesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi na kutoa mazingira mazuri ya kufundisha na kujifunzia.
Katika hatua nyingine Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhemeli Stella Silutongwe alisema walipokea kiasi cha shilingi milioni 47.6 na Halmashauri kuongeza kiasi ya milioni moja ambazo zimekabilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu matano ya vyoo na chumba maalumu choo kwa ajili watoto wa kike.
Alisema baada ya kukamika kwa mradi kuwapa nafuu walimu na wananfunzi ambapo hapo awali walilizimika kufundisha kwa awamu mbili kila siku kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.
MWISHO
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa