• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Nukushi ya malalamiko |
TABORA REGION ADMINISTRATIVE SECRETARY

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi Ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Biashara
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Mawasiliano
    • Muundo
  • Wilaya
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Wilaya ya Urambo
    • Wilaya ya Igunga
    • Wilaya ya Uyui
    • Wilaya ya Kaliua
    • Wilaya ya Sikonge
    • Wilaya ya Nzega
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Tabora
    • Halmashauri ya Manispaa ya Tabora
    • Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
    • Halmashauri ya Wilaya Urambo
    • Halmashauri ya Mji wa Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
    • Halmashauri ya Wilaya Sikonge
  • Fursa za Uwekezaji
    • Miombo Project
      • Miradi iliyokamilika
      • Miradi inayoendelea
    • Kilimo
      • Miombo Project
        • Miradi iliyokamilika
        • Miradi inayoendelea
    • Mifugo
    • Opportunity services
    • Viwanda na Biashara
      • New menu item
    • Madini
    • Uvuvi
    • EQUIP-TANZANIA
    • FURSA ZA UWEKEZAJI
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Tafiti
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

RC TABORA AAGIZA WAFANYABIASHARA KULIPA KODI KWA WAKATI ILI KUEPUKA FAINI

Posted on: September 15th, 2020

MKUU wa Mkoa wa Tabora Dkt. Philemon Sengati ametoa wito kwa wafanyabiashara,wananchi kulipa kodi kwa wakati ili kuepuka usumbufu na faini ambayo wanaweza kutozwa kwa wale wanaochelewa.

Alitoa kauli hiyo kwenye kikao cha waandishi wa habari na Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati akizungumzia kampeni inayoendelea mkoani hapa ya elimu kwa mlipakodi inayojulikana kama mlango kwa mlango.

Dkt. Sengati alisema kuwa kodi ndio inayoiwezesha Serikali kugharamia huduma za jamii ikiwemo kujenga vituo vya afya na kuboresha barabara na madaraja, utoaji elimu bure ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara ya watumishi wa umma.

Aliwataka wafanyabiashara mkoani Tabora kutoa ushirikiano kwa Maafisa wa TRA watakaopita katika shughuli zao za biashara wakifanya zoezi hilo la kutoa elimu ya kodi.

“Ninawaasa wafanyabiashara na walipakodi wote mkoani hapa kutoa ushirikiano kwa maafisa wa TRA na watumie elimu hiyo kama fursa ya kupata uelewa na kutoa maoni yao kwa ajili ya maboresho ya Sheria za Kodi”, alisema Dkt. Sengati.

Alisema kuwa Mamlaka ya Mapato imeamua kutoa elimu hiyo ili walipakodi wapende kulipa kodi kwa hiari na isionekane wanashinikizwa bali waone ni haki yao kufanya hivyo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua wafanyabiashara wote ambao watakutwa wakiuza bidhaa zao bila kutoa stakabadhi zinazotolewa kwa njia ya mashine za kieletroniki (EFD).

Naye Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Makao Makuu Diana Masalla alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni  kusikiliza maoni ya walipakodi kwa ajili ya kuboresha huduma za TRA na kuongeza walipakodi wapya.

Alisema kuwa wakati wa utoaji elimu hiyo watawakumbusha wananchi kulipa kodi stahiki na kwa wakati, kusikiliza kero na changamoto walizonazo na hatimaye kuzitafutia ufumbuzi.

Masalla alitaja maeneo ambayo wanakusudia kutembelea katika zoezi hilo la utoaji elimu kwa wafanyabiashara kuwa ni ni pamoja na  soko kuu la  Manispaa ya Tabora, Nzega mjini Igunga,  Choma, Nkinga na Simbo.

Alisema lengo ni kuwafikia wafanyabiashara 3,500 katika kipindi cha wiki moja watakayokuwa wakitoa elimu ya mlipakodi mkoani Tabora.

Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka Makao Makuu Dar es Salaam wakishirikiana na Maafisa wa TRA wa Mkoa wa Tabora wameanza kampeni ya elimu kwa mlipakodi iliyopewa jina la ‘’Mlango kwa mlango’’.

Kwa Mkoa wa Tabora, Kampeni hiyo imeanza tarehe 14 na itamalizika tarehe 19 Septemba, 2020.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA, 2024 December 18, 2023
  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE MACHI 8 March 07, 2024
  • BEI ELEKEZI YA MBOLEA YA CAN KWA KAMPUNI YA YARA June 15, 2022
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MITAALA YA ELIMU TANZANIA BARA March 23, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • “WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MSIMAME KWENYE MISINGI YA SHERIA NA HAKI.”: MHE. RWEBANGIRA

    July 15, 2025
  • DKT. RUTANISIBWA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA SIKU MBILI KWA MAKATIBU WA AFYA KUTOKA HALMASHAURI ZA MKOA WA TABORA:ASISITIZA UWAJIBIKAJI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI

    July 15, 2025
  • "UWAJIBIKAJI NA USALAMA KWANZA: PPRA KANDA YA MAGHARIBI NA KATI YAFANYA TATHMINI YA UTENDAJI KAZI NA KUTOA MAFUNZO YA KUKABILI MAJANGA YA MOTO TABORA"

    July 08, 2025
  • MHE. CHACHA AIPONGEZA TIMU YA UMISSETA MKOA KWA KUSHIKA NAFASI YA TATU KITAIFA

    July 01, 2025
  • Angalia zote

Video

VIJANA WAKAA MEZA MOJA NA RC MKOA WA TABORA
video nyingine

Viungio vya Haraka

  • Maelezo na fomu ya ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma
  • Guidelines for the use of ICT in government
  • Agriculture
  • MALALAMIKO,PONGEZI NA MAONI INGIA HAPA
  • Bofya hapa Eoffice

Tovuti Muhimu

  • Ikulu
  • Ofisi ya Rais-Tamisemi
  • Ofisi ya Rais-Utumishi
  • SALARYSLIP
  • Sekretarieti ya ajira
  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tabora

    S.L.P: 25 Tabora

    Simu: 026 2604058

    Mobile:

    Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa mara
    • Service
    • owner

Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa