Na Tiganya Vincent
RS-Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewawataka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO) kutengeneza chupa za vyoo kwa ajili ya kufungashia asali.
Alisema hatua itasaidia kulinda ubora wa asali ya Tabora ambayo inatokana na uepo wa mistu ya miomboi.
Balozi Dkt. Batilda amesema hayo leo wakati wa ziara yake ya siku moja katika Ofisi za SIDO Mkoa wa Tabora kwa ajili kukagua shughuli za Wajasiriamali wadogo ambao wanasimamiwa na Shirika hilo.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora ameitaka SIDO kushirikiana na Shirika la Posta kutangaza ndani nanje ya Nchi bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Wajasirimali Wadogo wanaowasimamia.
Amesema hivi sasa Posta wanaendesha biashara kwa njia ya mtandao na hivyo ni vema wakaangalia uwezekano wa kushirikiana nao ili kuwainua Wajasiriamali wao.
Naye Meneja wa SIDO Mkoa wa Tabora Samwel Neligwa amesema hivi sasa bidhaa nyingi zinazotengenezwa Wajasiriamali wao zinapatikana katika Matndao wao.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa