TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
|
OFISI YA MKUU WA MKOA WA TABORA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WANANCHI KUHUSU UJIO WA MWENGE WA UHURU TAREHE 26 AGOSTI 2019 MKOANI TABORA
Ndugu wananchi wa mkoa wa Tabora;
Ninayo heshima kubwa kuwajulisha kwamba, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa Mkoani Tabora kuanzia tarehe 26 Agosti hadi 2 Septemba 2019 katika halmashauri zote 8 za mkoa wa Tabora kwa ratiba ifuatayo:-
Na |
TAREHE |
HALMASHAURI |
1 |
26 AGOSTI 2019 |
IGUNGA DC
|
2 |
27 AGOSTI 2019 |
NZEGA MJI
|
3 |
28 AGOSTI 2019 |
NZEGA DC
|
4 |
29 AGOSTI 2019 |
UYUI DC
|
5 |
30 AGOSTI 2019 |
KALIUA DC
|
6 |
31 AGOSTI 2019 |
URAMBO DC
|
7 |
1 SEPTEMBA 2019 |
TABORA MANISPAA
|
8 |
2 SEPTEMBA 2019 |
SIKONGE DC
|
Katika kila halmashauri mkoani Tabora, Mwenge wa Uhuru utaweka Mawe ya Msingi, kufungua na kuzindua miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali za umma na binafsi.
Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 ni:-
“MAJI NI HAKI YA KILA MTUTUTUNZE VYANZO VYAKE NA TUKUMBUKE
KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA ”
Ujumbe huu unaambatana na kaulimbiu nyingine zisemazo:-
UKIMWI – “Pima, Jitambue, Ishi”.
Malaria – “Nipo tayari kutokomeza Malaria, Wewe Je?”
Rushwa – “Kataa Rushwa, Jenga Tanzania”.
Dawa za Kulevya – “Tujenge Maisha Yetu, Jamii yetu na Uhuru wetu bila Dawa za Kulevya”
Ndugu wananchi, Mwenge wa Uhuru katika mkoa wetu wa Tabora utatembelea miradi 39 yenye thamani ya Tshs 16,090,796,847.13 mkoa mzima.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zitaambatana na maonesho ya shughuli mbalimbali za ujasiriamali kutoka katika vikundi mbalimbali vya kiuchumi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Aidha kutakuwa na maonesho ya shughuli zinazofanywa na sekta mbalimbali za afya, maji na maelezo ya jinsi ya kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 2019.
Katika kila halmashauri kutafanyika mikesha itayohusisha shughuli za upimaji wa virusi vya UKIMWI, Malaria na magonjwa mengine usiku mzima. Hivyo; wananchi wote mnaombwa kushiriki kikamilifu kwa kujitokeza maeneo yote Mwenge wa Uhuru utakakopita na kuushangilia kwani ni alama muhimu inayowakilisha taifa letu popote duniani.
MWENGE WA UHURU OYEEE……!!!!!
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa