A. SEKTA YA MIFUGO
1.0 Idadi ya mifugo mkoani
Mkoa wa Tabora una changia idadi kubwa ya mifugo nchini. Mkoa unakadiriwa kuwa na idadi ya mifugo kama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapo chini:-
Jedwali Na.1(a) Idadi ya Mifugo Mkoani Tabora
H/shauri
|
Ng’ombe Asili
|
Ng’ombe kisasa
|
Mbuzi asili
|
Mbuzi kisasa
|
Kondoo
|
Kuku asili
|
Kuku kisasa mayai
|
Nzega DC
|
469,186
|
175
|
209,200
|
271
|
48,503
|
458,509
|
6,220
|
Nzega TC
|
79,295
|
615
|
34,232
|
603
|
6,968
|
56,698
|
11,377
|
Tabora MC
|
81,025
|
2,277
|
33,539
|
407
|
7,931
|
1,036,314
|
225,861
|
Igunga Dc
|
583,228
|
1,550
|
364,380
|
178
|
195,024
|
560,864
|
4,081
|
Sikonge DC
|
373,298
|
56
|
130,710
|
192
|
20,150
|
515,000
|
981
|
Urambo DC
|
128,085
|
213
|
53,232
|
26
|
10,572
|
19,293
|
2,123
|
Kaliua DC
|
564,836
|
104
|
91,771
|
0
|
17,441
|
227,708
|
7,154
|
Uyui DC
|
494,592
|
52
|
152,180
|
13
|
72,118
|
582,803
|
386
|
Jumla
|
2,773,545
|
5,042
|
1,069,244
|
1690
|
378,707
|
3,457,189
|
258,183
|
Chanzo: Halmashauri za wilaya, mji na Manispaa
Kasi ya kuongezeka kwa ngombe 1.6% kondoo na mbuzi 3.2% kwa mwaka.
Jedwali Na 1(b) Idadi ya mifugo mingine
H/shauri
|
Bata
|
Nguruwe
|
Punda
|
Mbwa
|
Paka
|
Sungura
|
Kanga
|
Nzega DC
|
6,595
|
1,173
|
954
|
9,870
|
2,153
|
0
|
0
|
Nzega TC
|
1,315
|
1,939
|
219
|
1,105
|
121
|
0
|
0
|
Tabora MC
|
2,943
|
13,741
|
235
|
4,648
|
392
|
0
|
0
|
Igunga Dc
|
5,181
|
5,102
|
11,055
|
9,182
|
3,642
|
53
|
0
|
Sikonge DC
|
110,900
|
3,113
|
602
|
15,404
|
3,694
|
31
|
896
|
Urambo DC
|
873
|
1,496
|
88
|
1,211
|
511
|
87
|
538
|
Kaliua DC
|
2,984
|
4,601
|
377
|
6,210
|
3,770
|
0
|
1,028
|
Uyui DC
|
74,161
|
739
|
896
|
7,510
|
3,072
|
0
|
0
|
Jumla
|
204,952
|
31,904
|
14,426
|
55,140
|
17,355
|
171
|
2,462
|
Chanzo: Halmashauri za wilaya, mji na Manispaa
Hivyo uwekezaji unaweza ukafanyika katika uzalishaji wa
2.0: Umhimu wa sekta ya mifugo
Nichanzo cha mapato kwa Halmashauri 8 za Mkoa wa Tabora na Serikali Kuu;
Ni chanzo cha Malighafi viwandani (maziwa, vyakula vya mifugo, Nyama na Ngozi);
Chanzo cha ajira rasmi na ajira zisizo rasmi;
Ni chanzo cha mbolea za asili mashambani;
Ni chanzo cha wanyama kazi kwenye shughuli za kilimo na shughuli za kusafirisha mizigo (mazao); na
Ni chanzo cha vyakula vya binadamu
3.0: Fursa zilizopo katika sekta ya mifugo
Uwepo wa mifugo mingi ambapo kwenye mnyororo wa thamani unazalisha malighafi zifuatazo:- nyama, maziwa, ngozi, mbolea, vyakula vya mifugo na pembe&kwato;
Uwepo wa ardhi ya kutosha ambayo ikifanyiwa mpango wa matumizi bora ya ardhi, Mkoa utafanya ufugaji wa kisasa na wenye tija;
Uwepo wa maji ya mvua naya ardhini; na
Uwepo wa watu ambao wako tayari kujishughulisha kiuchumi katika sekta ya mifugo.
Uwepo wa eneo lililotengwa la Luyembe lenye hekta 15,000 kwa ajili ya uanzishaji wa ranchi ya mifugo. Eneo hili lipo katika Kata ya Zugimulole katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua.
Uwepo wa eneo la ranchi ya Kisasiga lenye ukubwa wa hekta 42,000 ambalo lilikuwa ranchi ya mifugo.
B. SEKTA YA UVUVI
1.0: idadi ya mito na mabwawa
Katika Mkoa kuna jumla ya mito 11 na mabwawa 10 ambamo shughuli za uvuvi zinafanyika na jumla ya wavuvi 1,627 ndio wanaofanya shughuli za uvuvi katika vyanzo hivyo. Mabwawa, katika Mkoa ni Igombe na Kazima (Tabora), Mibono, Uluwa, Igigwa na Utyatya (Sikonge), Sagara (Kaliua), Loya (Uyui) na Mwanzugi na mbuga ya Wembere (Igunga). Shughuli za uvuvi hufanywa na wavuvi binafsi na kwenye vikundi vya ushirika.
Mkoa una jumla ya wafugaji 130 walio na jumla ya mabwawa 247 ya kufugia na pia kuna vikundi vinane (8) ambavyo vimeunda SACCOS na hivyo kuwa katika hali nzuri ya kupata mikopo na kujiendeleza zaidi
2.0: Kituo cha kuzalisha vifaranga wa samaki Wilaya ya Igunga
Kituo cha Mwamapuli kazi yake ni kuzalisha vifaranga vya samaki na kuvisambaza kwa wafugaji yakiwemo mabwawa ya Serikali (bwawa la Igombe na bwawa la kazima yalipokea vifaranga elfu 70), mabwawa hayo yapo Halmashauri ya Manispaa ya Tabora. Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, mabwawa ya Ulyanyama, Uluwa, Igumila na Igigwa yalipewa vifaranga vya samaki elfu 20 kutoka kituo cha Mwamapuli.
3: Fursa zilizopo katika sekta ya uvuvi
Uwepo wa mito na mabwawa
Uwepo wa bonde la Wembere katika Halmashauri ya Wilaya ya Igunga na Uyui ambalo huifadhi maji mengi na kuwezesha shughuli kubwa za uvuvi kufanyika.
Kituo cha kuzalisha vifaranga wa samaki Wilaya ya Igunga ambacho kinaweza kuzalisha vifaranga na kuvifuga kwa njia ya vizimba kwenye mabwa yaliyopo Mkoani Tabora.
Tabora
S.L.P: 25 Tabora
Simu: 026 2604058
Mobile:
Barua Pepe: ras.tabora@tamisemi.go.tz
Haki Miliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tabora .Haki zote zimehifadhiwa